Chapati Za Nyama
Chapati Za Nyama
Vipimo
Unga - 1 ½ vikombe vya chai
Mafuta - ¼ kikombe cha chai
Chumvi - ½ kijiko cha chai
Maji - 1 kikombe cha chai
Mafuta - ½ kikombe cha chai
Mayai- 6 mayai
Manda nyembamba za mraba (Spring roll pastries sheet) - 6
Nyama ya kusaga - ½ kilo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 1 kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwakatwa - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Pilipili mbichi - kiasi (ukipenda)
Bizari ya pilau ya unga - ½ kijiko cha chai.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya unga na mafuta ¼ kikombe maji na chumvi pamoja kanda mpaka ulainike
- Kata madonge sita, mimina mafuta ½ kikombe kwenye chombo kipana kisha yaroweke madonge kwa muda wa ½ saa hadi saa 1.
- Changanya nyama na vitu vyote na ichemshe mpaka iwe kavu kama nyama ya sambusa , wacha ipoe.
- Sukuma donge ulitandaze liwe jepesi, kisha weka juu yake hiyo manda nyembamba ya mraba .
- Kwenye bakuli ndogo piga yai moja na vijiko 2 vya hiyo nyama kavu kisha mimina juu ya hiyo manda ya mraba kisha ifunike kama inavyoonyeshwa kwenye picha.
- Choma kama unavyochoma chapati ila wakati unageuza kutia mafuta toboa toboa na uma ili yai lipate kuiva vizuri ndani kwa moto wa kiasi.
- Weka kwenye sahani tayari kuliwa.