Biriani Na Sosi Ya Nyama Ya Mbuzi
Biriani Na Sosi Ya Nyama Ya Mbuzi
Vipimo
Nyama Ya Mbuzi - 1 Kilo
Mchele - 4 Magi
Vitunguu - 3
Nyanya - 2
Nyanya kopo - 3 vijiko vya chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Garam Masala (mchanganyiko wa bizari) - 2 vijiko vya supu
Hiliki - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Mafuta - ½ kikombe
Zaafarani au rangi za biriani za kijani na manjano/orenji
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Sosi Ya Nyama
- Changanya nyama na thomu, pilipili, chumvi na nusu ya garam masala. Tia katika treya ya oveni uipike nyama (Bake) hadi iwive. Au iwivishe kwa kuichemsha.
- Katika kisufuria kingine, tia mafuta (bakisha kidogo ya wali) kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi, kisha tia nyanya, nyanya kopo, bizari zote nyingine zilizobakia.
Namna Ya Kupika Wali
Mchele - 4 magi
Mdalasini - 1 kijiti
Hiliki - 3 chembe
Kidonge cha supu - 1
Chumvi
- Osha na roweka mchele wa basmati.
- Tia maji katika sufuria uweke jikoni. Tia kidonge cha supu, mdalasini, hiliki na chumvi .
- Yakichemka maji tia mchele, funika upike hadi nusu kiini kisha uchuje kwa kumwaga maji.
- Tia mafuta kidogo katika mchele na zaafarani iliyorowekwa au rangi za biriani kisha rudisha mchele katika sufuria ufunike na upike hadi uwive.
- Pakua wali katika sahani kisha mwagia sosi ya nyama juu yake, pambia kwa kukatika nyanya, pilipili mboga na figili mwitu (Celery) au mboga yoyote upendayo.