Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ya Ng’ombe
Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ya Ng’ombe
Vipimo
Ndizi - 15 takriiban
Nayma ya ng’ombe - 1 kilo
Kitunguu maji - 1
Nyanya - 3
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi ilopondwa - 2
Jira/cummin/bizari ya pilau ilosagwa - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 1
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha nyama kwa ndimu, chumvi na tangawizi mbichi na kitunguu thomu.
- Menya ndizi na zikatekate vipande kiasi, weka katika sufuria.
- Katakata kitunguu na nyanya utie katika ndizi.
- Tia jira na chumvi.
- Nyama ikiwiva mimina pamoja na supu yake ufunike ndizi ziwive na kuwa tayari kuliwa.
- Ukipenda tia pilipili mbuzi zichemke pamoja na ndizi.