Kamtoroka Mume Kwa Sababu Anampiga, Nini Haki Yake Kuhusu Mahari Ambayo Hakulipwa Mwanawe?
SW
Assalam Aleikum. Mimi nimeolewa miaka mitatu na nusu na nina mtoto mmoja. Mimi na mume wangu tunaishi pamoja na familia yake. Lakini hatukuweza kusikizana nao. Ilifika wakati hadi mume wangu akanipiga. Niliweza kutorakea nyumbani kwetu maana ni mbali. Lakini mume wangu amekataa kuja nyumbani kutoa pole kwa yale aliyoyatenda na wazazi wangu wanadai aje kwanza. Nilimuacha mwanangu huko kwa vile sina uwezo
Hajalipa mahari yangu bado Je Kuna haki gani kwangu.
- Kwa mtoto wangu
- Kwangu mimi mwenyewe.
Naomba usaidizi tafadhali
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako, dada yetu kuhusu kupigwa na mumeo. Haya ni mashtaka ya upande mmoja na inakuwa ni vigumu sana kuweza kuamua kwa uadilifu lakini tutajaribu kugusia mambo mengi pamoja na kukuuliza maswali ili tuweze kukusaidia kwa njia ambayo ni nzuri zaidi.
Mwanzo inaonyesha kulingana na ibara ya swali lako ni kuwa mume ni tajiri kuliko familia yenu. Je, ulikubali kuolewa naye kwa sababu ya utajiri wake au nasaba yake? Ikiwa ulimkubali kwa msingi huo utakuwa umekosea
“Akikujilieni ambaye mmeridhia Dini na maadili yake, mwozesheni kwani mkitofanya hivyo kutakuwa na fitina na uharibifu mkubwa” (at-Tirmidhiy).
Kisha umefanya kosa la kukimbia kutoka katika nyumba yako. Hukueleza kwa kina sababu nyengine iliyokufanya ufanye hivyo (yaani kutoroka nyumbani kwako). Je, alikupiga mara hiyo hiyo moja au ni ada yake kukupiga? Je, ikiwa alikupiga siku hiyo moja tu, ulifanya kosa lolote? Tufahamu kuwa mume hafai kumpiga mkewe kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Si bora miongoni mwenu mwenye kumpiga mkewe”.
Lakini kosa
Kosa
“Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Allaah Atawawezesha. Hakika Allaah ni Mjuzi Mwenye khabari” (4: 35).
Ama kuhusu mahari ni haki yako na ulikuwa upatiwe kuanzia mwanzo lakini huku kukimbia kwako ndiko kunaleta utata. Je, unataka kujiachisha au humtaki tena mumeo au unatakaje? Kwa ajili ya hayo ambayo hukutueleza inabidi kuhusu
Tunamomba Allaah Aliyetukuka Awaondolee matatizo hayo na Awarudishe tena katika ndoa.
Na Allaah Anajua zaidi