Mume Wangu Ameoa Mke Wa Pili Ananidhulumu
SWALI:
Mimi ni mwanamke nimeolewa sasa karibu mwaka 17 na niko na watoto 5 tunaishi nchi ambayo sio ya kislamu mume wangu kamuwa niondoke hio inchi ikaende kusomesha watoto quran nanikafanya hivyo tukaenda pamoja akaniacha huko akarudi zake, nilipata taabu mwezi za kwanza lakini nilisubiri na huku kila siku namwambia twataka kurudi aliniambia nisubiri kumbe huko nyumbani ananidhulumu na kutembeya na mwanamke ambaye namjuwa, nilirudi haraka na akaniambia kama amesingiziwa, ndio nikashika mimba ya mtoto wangu watano, nilipitia mitihani nyingi sana mume wangu akamuoa huyo mwanamke na ana watoto kwa mume wa kwanza, nilisubiri sasa nishapewa talaka mbili, na mume wangu kanifaya mimi separate na haswali kabisa na ana nidharau nifanyeje. Plz I need help
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Mwanzo tunakushukuru kwa kuwa na Imani nasi kuwa tunaweza kukusaidia kwa tatizo ulilonalo. Nasi kama Waislamu hatuna budi kukupatia nasaha kwa ikhlasi kabisa kadri ya uwezo wetu.
‘Abdullaah bin Jariyr (Radhiya Allaahu ‘Anhu) anasema nilimbai Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah na kumpatia nasaha kila Muislamu (al-Bukhaariy).
Katika hayo uliyoyaeleza tunaona jambo ambalo lafaa kwako kufanya ni kumweka mume wako chini na muzungumze
Ikiwa hukupata natija yoyote katika mazungumzo hayo basi itabidi muitishe kikao ambacho wewe na yeye mtakuwepo pamoja na wawakilishi wako na wake yeye. Ikiwa kweli mnataka suluhu basi Allaah Aliyetukuka Atawafanikishia na natija nzuri itapatikana. Lakini ikiwa kukaa nyinyi wawili hapana faida kama wanandoa hamtafanikiwa katika
Jinsi ulivyosema kuwa mumeo haswali faida itakayopatikana kukaa pamoja haitakuwepo kabisa na kila wakati mtakuwa mnagombana. Jambo la busara hapa ni kutengana naye lkwani hakuna kheri yoyote kwa kuishi na mtu asiyeswali, lakini tunakushauri kwanza ufanye juhudi hizo za kutaka kumrekebisha.
Tunakutakia kila la kheri katika harakati hizo.
Na Allaah Anajua zaidi