Nimetuhumiwa Kuwa Mwizi Kwa Sababu Ya Kupokea Posho Kwa Kumpa Mtu Fursa Ya Kumuuzia Chakula Chake
SW
Asalam aleykum,
Nilikuwa treasurer wa waislamu, ila kabla ya hapo nilikuwa naendesha program binafsi ya kuwauzia chakula baadhi ya wanajumuiya hao. Nilipopata uongozi huo niliendelea na biashara hii kwani ilinisaidia. Ilinilazimu kumbadili mpishi ili kuboresha huduma.
Ilipofika Ramadhani mpishi wa mwanzo alinifuata ili nimpatie tender futari kama ilivyokuwa hapo nyuma ila nikamuambia nina mpishi mwingine, tuliongea na tukakubalina, atanipa kiasi fulani kwa kila sahani kama kwenye ile program binafsi. Futari ilianza kuletwa na mambo yalienda
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu posho mliyokubaliana na aliyekuwa mfanyi kazi wako.
Gogoro kama
Biashara Kiislamu ni maelewano baina pande mbili husika na baada kuelewana inabidi kila upande uwe ni wenye kutimiza mapatano hayo kwa kiasi cha juu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Waislamu wapo juu ya masharti (waliosikilizana)". Hivyo, ni wajibu kila upande utimize maagano maadamu hakuna haramu kati ya hayo maafikiano. Lakini mara nyingi huwa haiwi hivyo kwa kutojua uzito wa ahadi waliyoekeana baina
Katika mapatano hayo hakuna haramu yoyote kwani wewe umempatia fursa ya kuuza chakula chake katika sehemu yako. Ikiwa mama huyo hakutaka kuingia katika mapatano hayo anagekuambia kuanzia mwanzo ili kusiwe na mivutano
Hata hivyo, yaonyesha kuwa nawe una makosa kwa upande mwengine,
Na Allaah Anajua zaidi