Medical Insurance Halaal Au Haraam?
SWALI LA
Bismilahi warahmatulahi wabarakatu Asalamu Aleykum Warahmatulahi Wabaraakatu, Shukran kwa kazi kubwa munayofanya.
Ama swali yangu ni kuhusu medical insurance? Nilikuwa nataka kuweka mtoto wangu katika medical insurance ili akigonjeka walipe bill yake. Huwa wanaitisha alfu 25 kwa mwaka alafu wanalipa bill ya mtoto akikonjeka hata
SWALI LA PILI:
Bismillahi Rahmani Rahiim.
Shukran
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu uhalali au uharamu wa medical insurance.
Misingi ya insurance imejengwa katika uharamu hivyo kuifanya kuwa haramu katika sheria yetu ya Kiislamu. Insurance ni bahati nasibu na kwa ajili ya kutaka kupata faida nyingi huwa hawakubali mtu ambaye ana ugonjwa wa kudumu kujiandikisha.
Insurance ni bahati nasibu, kwa kuwa unaweza usiwe mgonjwa kwa mwaka mzima hivyo kufanya pesa zako ziwe zimepotea bila huduma ya aina yote. Uislamu haufanyi kazi aina hiyo, unataka mtu atoe pesa na apate huduma kutoka kwa shirika au kampuni au idara nyingine yoyote. Kisha pia katika insurance huwa kuna riba ndani yake na udanganyifu ambao umekatazwa na Uislamu.
Ikiwa kampuni ndio inalipa gharama ya wewe kwenda kutibiwa na hakuna njia nyingine utachukua insurance hiyo. Hata hivyo, ikiwa kampuni au shirika ni la Muislamu inafaa uzungumze na wakubwa kuhusu njia mbadala ya hiyo ya haramu. Na njia moja ni mwajiri kulipa tu wakati mfanyakazi ni mgonjwa na anapokwenda hospitali kutibiwa. Njia hii itakuwa ni afadhali
Na Allaah Anajua zaidi