Miti Ya Miashoki Ndiyo Iliyotajwa Katika Alama Za Qiyaamah?

 

Miti Ya Miashoki Ndiyo Iliyotajwa Katika Alama Za Qiyaamah?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalaam Alaykum

 

 

Naomba Kuuliza Kuhusu Kupanda Kwa Mti Huu Wa Muashoki {ni Mti Mrefu Sana Hapa Kwetu Watu Wengi Wameupanda} Maana Nasikia Ni Vibaya Katika Dini. Je Kweli Ni Haramu Au Watu Tu Wanasema?

 

 

Maana Mimi Ninao Nyumbani Kwangu Na Kama Vibaya Niukate

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Kwa jinsi tulivyofuatilia miti hiyo, inaonekana kufanana majina lakini hakuna ufanano wa maumbile ya miti hiyo baina ya ile inayoota Afrika Mashariki na ile inayoota Palestina. Ya Afrika Mashariki ni mirefu membamba isiyo na miba, ilhali ya Palestina ni mifupi mipana na yenye miba kama ilivyoelezwa katika Ahaadiyth. Na ndiyo haswa iitwayo Al-Gharqad na ndiyo iliyokusudiwa kwenye Ahaadiyth. 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta‘aalaa) Alitangaza kupitia kwa Nabiy Wake kuwa ardhi tukufu ya Palestina itatawaliwa na maadui au vitapiganwa vita ili kutekwa. Kwa ajili hiyo aliuhimiza ummah wake ufanye ribati hapo na kutekeleza amri ya Jihaad kuulinda ili usitekwe na maadui na kufanya juhudi kubwa za kuukomboa pindi unapoingia mikononi mwa adui. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametujulisha kuwa kabla ya Siku ya Mwisho kutatokea vita baina ya Waislamu na Mayahudi na kila kitu kitakuwa siku hiyo katika safu ya Waislamu hata mawe na miti. Kuhusu hili Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

عن عبد الله ابن عمر (رضي الله عنهما): ان رسول الله (صلى الله عليه وسلم) قال:  ((تقاتلون اليهود حتى يختبىء أحدهم وراء الحجر فيقول: يا عبد الله هذا   يهودى ورائى فاقتله))    وفى رواية قال: ((لا تقوم الســـــاعة حتى تقاتلوا اليهود)). وذكر باقى الحديث

 

Imepokewa na ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtapigana na Mayahudi mpaka mmoja wao atajificha nyuma ya mawe ambayo yatasema: ‘Ee mja wa Allaah, huyu Yahudi nyuma yangu muue". Na katika riwaya nyingine: "Hakitosimama Qiyaamah mpaka mpigane na Mayahudi". Ikataja baki ya Hadiyth kama ilivyo juu (Al-Bukhaariy). Hadiyth nyingine inasema:

 

عن ابى هريرة (رضي الله عنه): عن النبى (صلى الله عليه وسلم)، انه قال: ((لا تقوم الســـــاعة حتى يقاتلوا المسلمون اليهود فيقتلهم المســلمون حتى يختبىء اليهوديّ  وراء الحجر والشجرفيقول الحجر والشجر:يا مســـلم  يا عبد الله هذا يهدىّ خلفي تعال فاقتله، الاّ الغرقد فانه من شــجر اليهود.))

Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Qiyaamah hakitofika mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi. Mayahudi watakuwa wanauliwa na kujificha nyuma ya miti na mawe. Miti na mawe itasema: ‘Ee Muislamu, Ee mja wa Allaah, njoo nyuma yangu yupo Yahudi umuue ila mti wa Gharqad kwani huo ni mti wa Mayahudi." [Muslim].

 

Kuhusu mti huu wa Gharqad uliotajwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), inasemwa katika kitabu 'Min Kunuuzus Sunnah', uk. 75, kuwa, "Ni mti wenye miba mikubwa na inapatikana kwa wingi katika ardhi ya Palestina. Ni miongoni mwa miti miovu ambayo inafanana na uovu wa Mayahudi na sifa zao mbovu."

 

Mti wenyewe pia unakuwa mfupi na unapandwa sana na Mayahudi huko katika nchi ya Palestina ili ipate kuwasaidia wakati huo watakapopigwa na Waislamu.

 

Je, mawe na miti itazungumza kwa maneno yanayosikika? Na'am, hiyo itakuwa ni Aayah miongoni mwa Aayah, dalili na miujiza ya Allaah (Subhaanahu wa Ta‘aalaa). Na jambo hilo ni rahisi sana kwa Allaah Aliyetukuka na Mwenye Nguvu. Au yatatamka kwa ulimi wa hali ilivyo. Kwa maana kuwa kila kitu kitamchongea Myahudi na kumfichua alipojificha. Na maana yoyote inayochukuliwa; kwamba kila kitu kitakuwa upande wa Waislamu na dhidi ya maadui zao Mayahudi. Na bila shaka ushindi unakuja, na kuwa zile hekaya za (nguvu zisizotetereka) ambazo Mayahudi wanajigamba nazo hazitobaki daima.

 

Ingawa kuna aina nyingi za miti ya Miashoki au Miashoka, na utafiti wetu umetuonyesha kuwa huo unaofanana na Al-Gharqad ni mojawapo wa aina ya Miashoka, lakini hiyo Miashoka inayopandwa Afrika Mashariki si ile iliyokusudiwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu aliyotaja yeye ni kama ilivyoelezewa hapo juu kuwa, ni mti wenye miba mikubwa na inapatikana kwa wingi katika ardhi ya Palestina. Kwa vile imetajwa haswa kwa sifa hizo na khaswa kwa vile imekusudiwa hiyo mifupi mifupi inayopandwa Palestina basi hiyo inayopandwa Afrika Mashariki haihusiani nayo.

 

Kwa hiyo, tunaweza kusema kwamba mti wa Muashoki na Gharqad ni miti miwili tofauti, kwani huu wa kwanza ni mrefu usiokuwa na miba ilhali wa pili ni mfupi. Hivyo, hatuoni tatizo la kuipanda hiyo miti inayojulikana Afrika Mashariki kama Miashoki kama ulivyouliza katika swali lako juu. 

 

Tunawawekea picha za miti miwili hiyo kwa wale wasiouijua hiyo miti:

Aina mbili ya Al-Gharqad inayopandwa Palestina:

Aina ya kwanza:

 

Aina ya pili:

 

 

Miashoka inayopandwa sana Afrika Mashariki ni hii hapa chini:

 

 

Pia ukizingatia utatambua kwamba haingii akilini kuwa miashoka hiyo mirefu inayopandwa nchi za Afrika Mashariki ndio zilizokusudiwa kwa sababu shina lake ni refu na jembamba mno, haiwezekani kwamba mtu ataweza kujificha bila ya kuonekana.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share