Nini Maana Ya Talaka Ya Ilaa Vipi Inatolewa?

SWALI

 

 

Nini maana ya Talaka ya Ilaa.  Pia Talaka ya Ilaa hupatikana kwa mtu kuamua kujitenga na mkewe zaidi ya ...

 


 

JIBU

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Talaka ya Ilaa. Maana ya Ilaa ni kuapa. Aina ya kiapo hiki ni pale mume anaapa kuwa hatolala na mkewe kwa kipindi fulani, ima chini au zaidi ya miezi minne. Iwapo kiapo cha Ilaa kitakuwa chini ya miezi minne, mume anatakiwa kusubiri muda wa kiapo kisha ataruhusiwa kuingiliana kimwili na mkewe. Mke anatakiwa awe na subira na hawezi kumtaka mumewe, katika hali hii ya kumaliza kiapo chake kabla ya kwisha muda. Imenukuliwa katika Swahiyh Mbili kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliapa kuwa atajitenga na wake zake kwa muda wa mwezi mmoja, naye akafanya hivyo.

 

Iwapo muda wa Ilaa ni zaidi ya miezi minne mke anaruhusiwa katika hali hiyo kumtaka mumewe baada ya kwisha miezi minne, amalize Ilaa na amwingile kimwili. Ikiwa hatofanya hivyo basi anafaa ampe talaka, na ikiwa hataki basi itafaa mamlaka iingilie kati na kumlazimisha mume kumtaliki mkewe ili mke asidhurike.

 

Qadhiya hiyo inapatika katika Qur-aan kama Anavyosema Allaah Aliyetukuka:

 

Kwa wanaoapa kuwa watajitenga na wake zao, wangojee miezi minne. Wakirejea basi Allaah hakika ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. Na wakiazimia kuwapa talaka basi Allaah ni Mwenye kusikia na Mjuzi” (2: 226-227).

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share