Mume Ana Tabia Ambazo Mke Hafurahishwi Nazo Katika Tendo La Ndoa

 

SWALI:

 

Namshukuru Allaah subhanahu wataala kwa kuniwezesha kuandika haya machache. Swali langu ni kwamba mimi nimeolewa sasa bado wapya katika ndoa hii kama miezi miwili na kwa kwangu ni ndowa yangu ya pili.yeye mume wangu njo kwanza anaowa. Ni kwamba tunapokuwa katika hali yetu ya kufanya mapenzi huwa mume wangu anapenda sana kunichezea ama kutia ulimi wake sehemu zangu za nyuma ila hajawahi kunitajia jambo lolote chafu kama kuniingilia nyuma, kwa sababu anajuwa kitendo hicho nakichukia na hata yeye pia anakiogopa kwaajili ya Allaah. Illa nataka kujuwa je nimakosa anapo nifanyia huyo mchezo wakunilamba naulimi wake. mimi sipendi ila nashindwa kumwambia nampenda sana mume wangu. ila naona hajuwi kama nimakosa na mimi pia sijuwi ila sikitaki tu kitendo hicho. Naomba mnipe fatuwa nzuri ili niweze kumpa mawaidha tusije kuingia pabaya.maasalam mungu awabariki.

 

Nakatika romanz naweza kumwambia baadhi ya romanz ambazo sizipendi kama kupana ulimi awo kunitia vidole sehem za siri? hivyo vyote sivipendi nahajuwi.nisaidieni kabla na hii haijavunjika please

 

 

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukuran kwa swali lako kuhusu matendo ya ndoa.

Asli katika utendaji wa mas-ala yote ya maisha yetu ya kila siku ikiwemo mas-ala ya starehe baina ya mke na mume au hata namna ya kuingiliana kati ya mume na mke ni kumuiga na kumfuata Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na huko ndio hasa kuthibitisha kumpenda (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam); kwani yeye pia alikuwa na wake na bila ya shaka yoyote ile alikuwa akistarehe na kuingilia nao na kuna mapokezi yaliyopokewa na mafundisho kuhusu namna gani alikuwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ahli zake; na Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameletwa kwa lengo la kuigwa hata katika kustarehe mke na mume; hii ina maana kuwa tunahitaji tumuige hata katika hilo na katika yaliyopokewa hakuna hata moja hata la kutunga au kuzuwa –mawdhuu'- kuwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya hayo unayoyauliza na hata tukijaaliya kuwa yanaruhusiwa ni vyema tuelewe kuwa msingi wa dini ni mtu kuwa na hayaa na hayaa ni katika Iymaan na kama huna hayaa huo ndio mtihani.

Asli katika Uislamu starehe kati ya mke na mume ni halali na hakuna namna fulani au vipi. Hili ni katika yaliyonyamaziwa kimya na kuachiwa wanandoa wawili na Iymaan zao wachague namna ya kustareheshana bila ya kumuasi Mola isipokuwa pale palipoainishwa kuwa ni haramu, hivyo basi kama wewe na mumeo starehe ya kuchezeana hazikutoshelezeni na hamuko tayari kuvumbuwa namna nyengine ya kustareheshana isipokuwa hiyo unayosema: mume wangu anapenda sana kutia ulimi wake sehemu zangu za nyuma, basi ni vyema uelewe kuwa mcheza kisimani huenda akatumbukia na hilo ni tahadhari na kujiweka mbali na jambo ambalo lilisababishwa kuangamizwa watu wa Mtume Luut ('Alayhis Salaam). Ni bora kuliepuka kuliko kulikaribia kwani huelewi wakati gani Shaytwaan ataweza kukupendekezeeni na kukushaurini kutenda tendo ambalo ni la haramu kama la kuingiliana nyuma.

 

Ndugu yetu, miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kuwa wazi kati ya mume na mke wakioana ni kila mmoja wao kumueleza mwenzake nini anapenda na nini hapendi ili waweze kuishi kwa raha na starehe na kama wewe kweli kama unavyosema kuwa: anajuwa kitendo hicho nakichukia na hata yeye pia anakiogopa kwa ajili ya Allaah, na ikiwa ni hivyo kama unavyosema, sasa kwanini mnakifanya kitu kitachopelekeni kukufikisheni huko? Na kwanini wewe unakubali kufanyiwa jambo ambalo una mashaka nalo na huna raha nalo? Na hali matendo ya ndoa yanahitaji maridhiano ya pande mbili na maridhishano.

 

Na kuhusu uliyosema kuwa: Na katika romanz naweza kumwambia baadhi ya romanz ambazo sizipendi kama kupana ulimi au kunitia vidole sehemu za siri? Sasa kwanini usimwambie ikiwa mnapendana na mnataka kuridhishana basi asitafute namna nyengine za starehe zitakazowaridhisha pande zote mbili? Ikiwa mtakubaliana na atakuelewa basi bila shaka mtakuwa na furaha nyote katika tendo hilo na katika maisha yenu kwa ujumla.

 

 

Hivyo, ni waajib wako kumfahamisha kuliko kukaa kimya ukidhani kumwmabia utamuudhi au mapenzi yatapungua na hali tayari yanaanza kupungua kwa kuchukizwa kwako na matendo yake kwako katika mas-la ya ndoa.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share