Vipi Afanye Kitendo Cha Ndoa Na Mke Mwenye Ukimwi?

SWALI:

 

Mimi niko na swali nauliza mfano kama unaishi na mke wako alafu mke wako anaumwa ukimwi wewe auna unaruusiwa kuishi naye ao vipi na ukifanya naye mapenzi kwa jiya ya kondom. Napendelea munitumie majibu kwa anuani hii ******** nikitegemea tapata ufafanuzi kwa kirefu juu niswali muhimu


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kufanya mapenzi na mke mwenye UKIMWI. Kabla hatujajibu swali lako ni muhimu nasi tupate baadhi ya maalumati kutoka kwako ili tuweze kukusaidia kwa njia iliyo nzuri.

 

Je, huyu mke alipata UKIMWI kwa njia gani? Je, alitoka nje na kuzini au alipata kwa njia nyingine isiyo ya zinaa? Ikiwa uko na mke naye alipata kwa njia ya zinaa huyo si mwenzi wako ambaye unaweza kumuita mke. Inatakiwa uzungumze naye atubie na arudi katika njia ya Allaah Aliyetukuka na Uislamu kikamilifu. Ikiwa ataomba msamaha kwa ajili ya Allaah Aliyetukuka na kuahidi kutorudia na hiyo ndiyo mara ya kwanza unaweza kumsamehe. Baada ya kumsamehe unaweza kubaki naye au ukamuacha. Hapo wewe ndio utakuwa muamuzi kwani wewe unamjua yeye kwa ndani zaidi kuliko sisi.

 

Ikiwa mkeo amepata ugonjwa huo kwa njia nyingine isiyokuwa ya zinaa kama vile kutiwa damu au katika kung'olewa jino au kuambukizwa kwa njia nyonginezo, basi hapo inafaa ukae na mkeo kwa wema. Inatakiwa umhudumie kwa njia nzuri. Hata hivyo, unatakiwa uchukue tahadhari ya hali ya juu sana na musiwe ni wenye kufanya kitendo cha ndoa pamoja naye. Madaktari wamekuwa ni wenye kuwahimiza watu katika hali hiyo watumie kondomu lakini utafiti unaonyesha kuwa unaweza kupata UKIMWI katika hali hiyo ya kondomu vilevile.

 

Nasaha yetu ni kuwa unaweza kuoa mke mwengine ili upate kuhakikisha ya kwamba utabaki katika utohara na kuwa mbali na zinaa na huku unamhudumikia mkeo katika hali hiyo. Unaweza kutangamana na mkeo katika kila jambo kama kula pamoja, kumshika ikiwa sehemu hiyo hana kijeraha, kulala naye ila kitendo cha ndoa kwa tahadhari usije nawe ukaambukizwa ugonjwa huo.

 

Maelezo zaidi soma yafuatayo:

 

Vipi Tuishi Na Muislamu Mwenye Ukimwi?

 

Mke Wake Ana Ukimwi Je Aendelee Kuishi Naye?

 

Kumuoa Mwanamke Mwenye Hiv Bila Ya Kufanya Kitendo Cha Ndoa

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share