Anaweza Kumuingilia Mkewe Katika Muda Anaonyonyesha Au Haifai?
SWALI:
Assalaam Aleykum Mimi ni kijana wa kiislam nimeoa nina mtoto mmoja .Swalilangu ni je inafaa kumwingilia mke wangu wakati ana mtoto wa miezi mwili na kama haifai ni inafaa baada ya muda gani? 2 Je ni kweli kwamba kufanya
jimai wakati mke ananyonyesha kunamuathiri mtoto? WABILAH TAWFIQ
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tumepokea Swali lako, na ingawa zamu yako haikufika bado ya kujibiwa kwa sababu kuna maswali mengi nyuma yako yaliyoingia, tunakujibu haraka kutokana na umuhimu wa Swali wa kujizuia haki yako kwa jambo ambalo sio kweli.
Umefanya vizuri kuuliza jambo
Hakuna makatazo ya kutokumuingia mke akiwa na mtoto mchanga au akiwa katika muda wa kunyonyesha. Unaweza kumuingilia mkeo wakati wowote ule pale tu akisita damu yake ya nifaas. Inampasa afanye ghuslu (kuoga josho) kwa maana ajitie twahara hata ikiwa ni siku chache baada ya kujifungua madamu damu imesita basi ameshakuwa ni mwenye kupasi kuswali, kufunga na mumewe anaweza kumuingilia wakati wowote apendao.
Ingia katika viungo vifutavyo upate maelezo zaidi kuhusu mas-ala haya.
Muda Wa Kutwaharika Na Damu Ya Nifasi
Na Allaah Anajua zaidi