Mume Ana Ukimwi, Alimtoa Mke Katika Ukiristo, Mke Kajua Dini, Lakini Mume Kamkatisha Tamaa Kwa Kukosa Maadili Na Uaminifu
SWALI:
Assalaamu 'alaykum
swali langu ni Mimi nimeolewa na nilikuwa Mkristo na kuslimu baada ya kutaka kuolewa na mme wangu ambaye ni Mwislamu, na mimi nikajitahidi kufuata dini jinsi inavyotakiwa kima vazi (Hijaabu), swala mara 5, swala za usiku, kujifunza kusoma Qur`an mpaka Mwenyezi Mungu akaniwezesha na kuanza kuwafundisha watoto wangu kidogo dogo.
Mme wangu kwa bahati mbaya akaanza kuumwa ugonjwa mbaya ukimwi inasikitisha
NIKAENDA NA MIMI KUCHUNGUZWA AFYA YANGU NA NIKAONEKANA SINA (NEGATIVE) NA NIKAAMBIWA NIENDE TENA BAADA YA MIEZI SITA . CONTROL YANGU IKAWA TENA SINA (NEGATIVE), SASA NIMIMALIZA.
SASA DAKTARI WANGU ALINIAMBIA SIO LAZIMA KUMUACHA LAKINI NITUMIE KONDOM; LAKINI MIMI SASA SITAKI TENA NAYE TENDO LA NDOA HATA KAMA ATATUMIA CONDOM NIKIFIKIRIA TU UKIMWI SINA HAMU KABISA. KWANI NASHIKWA NA UOGA. NA SASA NIMEJITENGA CHUMBA.
(1) SASA JE NIKIENDA KWA SHEHE KUOMBA TARAKA JE NI DHAMBI?
(2) AU NITAMUAIBISHA?
HUYU MME GANI KUONYESHA MFANO KAMA HUU KWANGU, UKIANGALIA ALIKONITOA KWENYE DINI NYINGINE?
NISAIDIENI NIPATA KUJUA KWANI SIFAHAMU KABISA NA INAPASHWA NIJUE
Ahsanten,
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mahusiano kwa wakati huu na mumeo.
Mwanzo tunakuombea
Kwa hali uliyo nayo tunataria kuwa utakuwa na daraja kubwa mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Ni ajabu kuwa mume ambaye ni Muislamu ataasi na kumuacha aliyesilimu kumshinda katika Imani na matendo mema. Hata hivyo, mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hakuna ajabu na aliyeingia katika Uislamu akiwa mtu mzima anaweza kuwa na daraja kubwa kuliko aliyezaliwa katika Uislamu. Na tunatarajia kuwa wewe utafikia daraja hiyo na zaidi.
Ama kuhusu migogoro au sintofahamu kwa wanandoa, Uislamu umeweka njia ya kuweza kutatua ili
Nasaha ambazo tunaweza kukupatia ni
1. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ni lazima
2. Ikiwa suluhisho limepatikana itakuwa kheri kwenu nyote, lau ikiwa amekataa basi itabidi uite wawakilishi wake, na wako na wewe na yeye muwepo katika kikao. Kwani jambo
3. Itabidi uende kwa Qaadhi au Shaykh, kujieleza yako naye mumeo ataitwa kuja kujieleza na kisha hukumu kutolewa. Magonjwa yasiyotibika kwa upande wa mume ni sababu ya kuweza kumfanya Qaadhi kuwaachisha wanandoa.
Tunakutakia kila la kheri katika mtihani wako huo.
Na Allaah Anajua zaidi