Mume Kahama Chumba Kwa Miezi 3 Hafanyi Tendo La Ndoa, Akiulizwa Anasema Anachoka Kazini

SWALI 

 

asalaam alaikum

nilituama maswali yangu wiki iliyopita naona bado sijapata jibu kuhusu mume wangu anavyoninyanyasa na hatuishi kama mtu na mume wake ndani ya nyumba yeye analala kwake na mimi chumba changu bila sababu na hata kitendo cha ndoa inafika muda wa mienzi 3 or 4 kila nikimhitaji ananiambia yeye sio robort sasa katika sheria ya dini itakuaje? na mimi nimestahmaili muda wa miaka 8 sasa maisha yangu yote kama hivi sina haki kwake kama mkewe,sasa nilikuwa naomba msaada wenu nifanye nini?  

 

mimi ……  nilikuwa nataka kufahamu vizuri kuhusu ndoa yangu,mimi na mume wangu kuna matatizo fulani hataki kuwa na mimi kwenye kitendo cha ndoa amehama chumba muda wa miwnzi 3 on and off sifahamu kwa nini nasema nae ananijibu anachoka kwa kazi sasa kidini inakuaje si mara ya kwanza tangu tuoane miaka 8 kama tabia sasa tafadhali nisaidieni hii ndoa gani mpaka sasa sijijui vipi maisha yangu naona siyafaham na umri unapotea nimevumilia sana almost 7yrs naona hakuna mabadiliko so nimewauliza swali langu nashukuru mmenijibu kuwa mtanfahamisha. sasa ndugu zanguni naomba mnisaidie maswala yangu naona sijifahamu shukran salaam alaikum


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Moja katika haki ya mke na mume ni kuingiliana na kama ulivyosema,  mimi na mume wangu kuna matatizo fulani hataki kuwa na mimi kwenye kitendo cha ndoa amehama chumba muda wa miezi 3 on and off sifahamu kwa nini nasema nae ananijibu anachoka kwa kazi.   Basi elewa kuwa katika ndoa hii kuna tatizo la kimsingi la watu kutakiwa kuoana. Na utatuzi wake ni kuwa kama huyo mume baada ya kuwa na kazi ambayo inaonyesha imemvunja na kufikia kuwa hawezi kukutimizia  haki yako  basi mke unayo haki ya kudai talaka kwani huenda ukajikuta    katika maasi  kwa kutamani kuingiliwa.   Ikiwa mwenye uhalali huu hana uwezo na si lengo la ndoa katika Uislamu kukaa mwanamke chini ya mwanamume asiyeweza kumuingilia. Na kama tatizo ni kuchoka kwa maana ya kuchoka tu basi msharui  mumeo  apunguze muda wa kazi au atafute kazi nyengine itayomuwezesha kuweza kuifanya kazi ya kumuingia mkewe kwani hiyo pia ni katika kazi anazotarajiwa kuzifanya.

Ikiwa umeshindwa kumshauri mwenyewe basi tafuta jamaa zako na jamaa zake ushitaki hali yako upatiwe suluhisho.

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share