Anampenda Sana Mume Wake Lakini Hawana Raha Katika Tendo La Ndoa, Wafanyeje?
SWALI:
A'laykum.
Mimi nina matatizo katika ndoa yangu hatuna hamu ya kufanya tendo ila tunafanya kwa ada tu ya ndoa. Hatusisimkwi katika tendo huwa hakuna raha ya aina yoyote kati yetu. Mimi huwa sijawahi kusikia raha hata mara moja na pia mume wangu amenithibitishia
Naomba kwa ajili ya allah munieleweshe nini nifanye kwa huyu mume mimi nampenda mume wangu
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumpenda
Furaha ni kwetu kwa kutuelezea kwa uwazi bila kuficha tatizo mlilo nalo. Matatizo kama hayo hutokea katika maisha ya ndoa baina ya wanandoa. Zipo sababu nyingi ambazo hupelekea
1. Huenda mume aliingia katika ndoa bila kuwa tayari au kutayarishwa katika
2. Huenda kuwa alichaguliwa bila mwanzo kuwa alikuwa na hamu ya kukuoa.
3. Huenda ya kuwa mume na mke hawajafahamu cha kufanya katika tendo la ndoa.
4. Kukifanya kitendo hicho kuwa ni ada na sio Ibaadah.
5. Huenda mume ana ugonjwa ambao unamfanya asiwe na raghba ya kitendo hicho.
6. Huenda mume amefanyiwa sihri na hivyo kutakiwa kufarakanishwa na mkewe kwa sababu moja au nyingine. Au huenda ikawa ni hasad.
Yale yanayotakiwa kufanywa kuhusu matatizo yanayowakumbwa ni kujaribu kwa kiasi kikubwa kufanya yafuatayo:
1. Ikiwa aliingia katika ndoa bila kuwa tayari au alichaguliwa bila kupenda ajitayarishe na akuridhie kwa Niyah
2. Huenda ikawa hampati starehe kwa kuwa hamjajaribu kupata maelekezo ya Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu raha hiyo. Kinachotakiwa ni kujitayarisha kwa kitendo hicho kila mmoja kwa mwenziwe. Na huko ni kuoga mkawa
3. Mnatakiwa mfahamu kuwa kitendo hicho si ada bali ni ‘Ibaadah
4. Muwe mnasoma Qur-aan kwa wingi na huku katika nyakati za kujibiwa muwe mnamuomba Allaah Aliyetukuka Awaondolee tatizo
.
5. Aende mume akasomewe na Shaykh ambaye ni mchaji Mungu na kisomo cha kishari’ah ili ibainike
Kwa kufanya hayo tunaamini kuwa kwa uwezo wa Allaah Aliyetukuka atakuwa ni mwenye kupona na kuwa katika hali njema na nzuri inshaAllaah.
Na Allaah Anajua zaidi