Mja Mzito Asome Surah Gani Ili Imsaidie Katika Kuzaa?
SWALI LA
Assalam alaykum warahamtu llahi wabarakatu.
Shukurani zote zinamstahi Allah, Muumba wa kila kitu mbinguni na ardhini.
Ndugu zangu katika Uislam napenda kuuliza suala langu
wabillahi taufiq
SWALI LA PILI:
Assalamu'alaikum Warahmatullahi Wabarakatuhuu.
Swali langu ni : nina mdogo wangu anatarajia kujifungua mwezi huu insha’Allah, sasa je kuna sura yeyote ile ambayo ataweza kusoma pindi uchungu utakapomuanza ili ajifungue kwa salama salmini?na je
wabillah tawfiq
JIBU
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hakuna Surah maalumu ya kusoma kipindi mwanamke yuko katika uja uzito, bali anaweza kusoma Qur-aan Surah yoyote ile.
Wanawake wengi wana itikadi kwamba mja mzito asome Surah Maryam kwa vile imetaja uja uzito wa Maryam (‘alayhas-salaam) na kuzaa kwake. Hakuna ushahidi kwamba wa jambo
Maelezo zaidi bonyeza kiungo kifuatacho:
Yanayopasa Kufanywa Na Mwenye Mimba Na Baada Ya Kuzaa
Na Allaah Anajua zaidi