Samaki Wa Kuoka Wa Rojo Viazi Na Bilingani Ya Kukaanga
Samaki Wa Kuoka Wa Rojo Viazi Na Bilingani Ya Kukaanga
Vipimo
Samaki Kolekole au changu mkubwa - 1
Bilingani - 1 kubwa
Viazi - 3
Tomato paste - 1 kikopo kidogo
Nyanya freshi - 2 kubwa
Kitunguu maji - 1 kikubwa
Kitunuu saumu (thomu/galic) iliyosagwa - 1 cha supu
Tangawizi - 1 cha chai
Pilipili manga - 1 cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu
Masala ya samaki - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Chumvi - Kiasi
Mafuta ya masala - 1/3 kikombe
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Msafishe samaki vizuri na mpasue pasue na kisu sehemu ya mnofu ili viungo viweze kuingia ndani na awive vizuri
- Changanya masala ya samaki pamoja na chumvi, thomu, tangawizi, pilipilipi mbichi, ndimu kisha mpake samaki vizuri akolee. Mroweke kwa muda wa saa tu hivi.
- Muweke samaki katika grill kwa moto wa wastani. Akiwiva juu, mgeuze upande wa pili.
- Samaki akiwa tayari kuiva basi mtoe na muweke kando
- Katakata bilingani na viazi vipande vipande vya duara.
- Weka kikaango jikoni na tia mafuta na subiri mafuta yapate moto. Kisha kaanga kwanza bilingani, zikiwiva na kugeuka rangi toa chuja mafuta, weka kando.
- Kaanga viazi pia, chuja mafuta weka kando.
- Weka sufuria jikoni na tia mafuta na yakipata moto tia kitunguu na kanga hadi kuwa hudhurungi
- Kisha tia nyanya freshi kaanga kwa muda na tia tomato paste na chumvi na pilipili manga kidogo
- Chukua chombo kama sahani kubwa ya shepu ya yai (oval shape) Weka kwanza samaki. Kisha mwagie rojo la nyanya. Kisha pambia bilingani na viazi pembeni, akiwa tayari.