'Aqiyqah: Anaweza Kujifanyia Mwenyewe Ukubwani Ikiwa Hakufanyiwa Na Wazazi Wake?
SWALI:
Assalam Aleykum warahmatullah taala wabarakatu
Namshukuru Allah Subhana Wataala kwa kutupa uzima na kuwajaalia kuwape elimu hii inayotusaidia katika dunia hii na huko mbele tuendako, hakika Mola awajaalie na awazidishie kila la kheri na kuwaondolea mitihani ya kidunia....na afya njema ili wengine tuendelee kuneemeka / kupata elimu hii.
Ndugu zangu waislamu. Swali langu linahusiana na Aqiyqa...
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu 'Aqiyqah. Wanachuoni wameelezea kulingana na Hadiyth zilizo Sahihi kuwa inapendeza kufanya 'Aqiyqah siku ya saba. Hata hivyo, ikiwa haikuwezekana kwa sababu moja au nyingine na hasa kutokuwa na cha kufanya 'Aqiyqah basi wakati wowote mwingine
Kwa minajili hiyo ikiwa utakuwa na uwezo wewe mwenyewe unaweza kufanya 'Aqiyqah.
Zaidi bonyeza viungo vifuatavyo:
Utaratibu Wa 'Aqiyqah Katika Sunnah
Kufanya Aqiyqah Ni Lazima Au Sunnah?
Nani Mwenye Jukumu la Aqiyqah?
Na Allaah Anajua zaidi