041-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kurefusha Kikao Baina Ya Sajdah Mbili, Adhkaar Na Kuinuka Kwa Kutegemea Mikono
KUREFUSHA KIKAO BAINA YA SAJDA MBILI
Pia, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikirefusha - hichi kikao baina ya sijida mbili- kiasi cha kukaribiana na urefu wa Sajdah yake([1]
), na mara nyingine, alibakia katika (kikao hiki) mpaka mtu akasema: "Amesahau".([2]
)
ADHKAAR BAINA YA SAJDAH MBILI
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kikao hiki akisema:
1-
Allaahumma [Rabbi] ghfirliy, warhamniy, [wajburniy, [warfa’niy], wah-diniy [wa’aafiniy], war-zuqniy]
Ee Allaah! [Ee Mola Wangu!] Nisamehe, na Unirehemu, na [Uniunge], na [Uniinue], Na Uniongoze, [Na Unipe afya] na Uniruzuku([3]
). Na mara nyingine akisema:
2-
Rabbi ghfirliy ighfirliy
Ewe Mola wangu! Nisamehe, Nisamehe([4]
). Na alikuwa akizisoma zote hizo mbili katika Swalah ya usiku.([5]
)
SAJDAH YA PILI
Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akileta Takbiyr na Sajdah (kwa mara) ya pili([6]
). Pia alimuamrisha aliyeswali vibaya kufanya hivyo. Alimuambia baada ya kumuamrisha kutulia baina ya Sajdah mbili
). Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akinyanyua mikono yake pamoja na Takbiyr mara nyingine.([8]
)
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akifanya katika Sajdah hii –Sajdah ya pili- (sawa sawa)
Kisha, alinyanyua kichwa chake huku akileta Takbiyr([9]
), na alimuamrisha aliyeswali vibaya kufanya hivyo, akimuambia baada ya kumuamrisha kusujudu (kwa mara) ya pili kama ilivyotangulia: ((….kisha nyanyua kichwa chako na sema 'Allaahu Akbar'))([10]
). Akamuambia: (([…kisha fanya hivyo katika kila rakaa (na Sajdah], (kwani) utakapo fanya hivyo, basi Swalah yako itakamilika, na ukipunguza chochote kile katika hayo, basi Swalah yako itapungua)).([11]
) Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akinyanyua mikono yake([12]
) mara nyingine pamoja na Takbiyr.
KIKAO CHA KUPUMZIKA
Kisha, anakaa sawa sawa (juu ya mguu wake wa kushoto sawa sawa mpaka kila mfupa unarudi katika sehemu yake).([13]
)
KUTEGEMEZA MIKONO MIWILI KATIKA KUINUKA KWA AJILI YA RAKAA (INAYOFUATIA)
Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiinuka huku akiitegemea ardhi kuelekea kwenye rakaa ya pili (akijisaidia kwa (kukamata) ardhi)([14]
). Pia alikuwa akiifumba ngumi (yake)([15]
) katika Swalah akiitegemea kwa mikono yake anapoinuka.([16]
)
[1]
Al-Bukhaariy na Muslim.
[2]
Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. Ibn Al-Qayyim amesema: "Sunnah hii imeachwa na watu baada ya zama za Maswahaba. Lakini anayefuata Sunnah na haangazi kwengine kunakoipinga, hana wasiwasi wa kupinga uongofu.”
[3]
Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na Al-Haakim, ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali.
[4]
Ibn Maajah ikiwa na isnaad nzuri. Imaam Ahmad amechagua kuiomba na hii; Is-haaq bin Raahawayh amesema: "Akipenda aseme mara tatu au aseme 'Allaahumma-ghfir-liy', kwa sababu zote mbili zimeripotiwa kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) baina ya Sajdah mbili". (Masaail ya Imaam Ahmad na Is-haaq bin Raahawayh kama ilivyosimuliwa na Is-haaq Al-Marwaziy Uk.19).
[5]
Hii haikanushi kutekelezwa nyiradi hizi katika Swalah za Faradhi kwa sababu ya kuweko tofauti baina ya hizo na Swalah za Naafilah. Hii ni rai ya Ash-Shaafi'iy, Ahmad na Is-haaq ambao wameona kwamba hizi zimeruhusiwa katika Swalah zilizofaridhiwa na za Sunnah
[6]
Al-Bukhaariy na Muslim.
[7]
Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali. Ziada ni kutoka kwa Al-Bukhaariy na Muslim.
[8]
Abu 'Awaanah na Abu Daawuud ikiwa na sanad mbili Swahiyh. Kunyanyua mikono huku kumetiliwa nguvu na Ahmad, Maalik na Ash-Shaafi'iy katika usimulizi wao. Taz. Tanbihi ya nyuma katika Sujuud.
[9]
Al-Bukhaariy na Muslim.
[10]
Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali.
[11]
Ahmad na At-Tirmidhiy ambaye amekiri ni Swahiyh.
[12]
Taz. Tanbihi ya nne ya mwisho.
[13]
Al-Bukhaariy na Abu Daawuud. Kikao hiki kinajulikana kwa Maulamaa wa Fiqh
[14]
Al-Bukhaariy na Ash-Shaafi'iy.
[15]
[16]
Abu Is-haaq Al-Harbiy kwa isnaad isiyo na makosa. Na maana yake inapatikana kwa Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh. Ama kuhusu Hadiyth: "Alikuwa akiinuka kama mshale bila ya kujisaidia kwa mikono yake", hii ni Hadiyth ‘mawdhwuu’ (Kutungwa) na usimulizi wote wenye maana