Kasisimkwa Ndani Ya Swalaah Nini Hukumu Ya Swalaah Yake?

 

ASsalamu alayka sheikh nauliza swali kama ifuatavyo Kuna kijana mmoja aliwahi kuniuliza SWALI: kuwa yeye aliswali swala ya faradhi, ghafla alijikuta misuli yake ya uume (dhakari) imesimama. Je kijana huyu alipaswa kuendelea na swala au swala yake imeharibika?

 


 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kusimika katika Swalah.

 

 

Hakika ni kuwa kusimama kwa misuli ya uume haivunji Swalah, hivyo kuendelea kwake katika kumaliza hiyo Swalah ndio sawa.

Hata hivyo, ikiwa ndani ya Swalah, ya faradhi au ya Sunnah atakuwa ni mwenye kufikiria kuhusu kitendo cha ndoa mpaka dhakari ikasimama Swalah yake itakuwa ni sahihi japokuwa thawabu za Swalah hiyo zitapungua.

 

Swalah itaharibika tu ikiwa kwa kusimama kwa dhakari atatokwa na maji.  Yakiwa ni madhii au manii. Bila shaka ikiwa ni madhii itabidi avunje Swalah akaoshe sehemu ya nguo ambayo imeingia maji hayo pamoja na kuosha dhakari yake.

Na yakiwa ni manii yaliyomtoka itabidi aende akaoge ndio kisha arejee kuiswali tena Swalah hiyo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share