Wameswali Kabla Ya Wakati Wake, Nini Hukmu Ya Swalah Yao?

Wameswali Kabla Ya Wakati Wake, Nini Hukmu Ya Swalah Yao?

 

 

SWALI:

 

Assalam Aleikum Warahmatullahi Wabarakatu.

 

Sisi tunaishi Ireland, huku tunaswali kufuata timetable kwani hatusikii muadhin. Niliset time ya alfajiri kuswali, Alhamdullillah niliamka nikaswali. Nilipomaliza nikamuamsha mume wangu na yeye akaswali pamoja na binti yangu (yuko na miaka minane). Tukarudi kulala kwani ilikuwa sio siku ya kazi. Tulipoamka binti yangu akatujulisha kama tumeamka na tumeswali one hour before alfajir. Nikatafuta kwenye Al-Bukhari lakini hakuna mahali panaposema chochote kuhusu kuswali kabla ya time na tufanye nini.

 

Naomba unijulishe ili ikitokea tena tujuwe tufanye nini. Jazakallah-ul-kheir.

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho 

 

 

Hakika ni kuwa Swalaah ni ‘Ibaadah kama ‘Ibaadah nyingine ambayo inategemea wakati. Kuingia wakati ni mojawapo ya sharti ya Swalaah, kumaanisha kuwa lau utaswali kabla ya wakati basi Swalaah haitoswihi. Kwa hiyo, Allaah ('Azza wa Jalla) Anasema:

 

 

فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ﴿١٠٣﴾

Mtakapomaliza Swalaah, mdhukuruni Allaah msimamapo, na mkaapo na mnapolala ubavuni mwenu Mtakapopata utulivu, simamisheni Swalaah (kama desturi), hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu.  [An-Nisaa [4: 103]

 

Kwa hivyo, ukiswali kabla ya wakati inatakiwa uiswali tena Swalaah kunapoingia wakati kwani Swalaah yako haikusihi. Inatakiwa muwe waangalifu sana kuhusu hilo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share