Kwa Nini Haiwezekani Mke Na Mume Kurudiana Baada Ya Talaka Tatu?
SWALI:
Aslm alkm
Swali langu ni kwa nini tumeamrishwa na mola kuwa ukishatowa talaka tatu hufai kumregea mtalaka wako mpaka aolewe na mume mwengine kisha apewe takala ndio wewe uweze kumuowa tena?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu sababu ya kutowezekana kumrudia mke baada ya talaka tatu.
Allaah Aliyetukuka Anatuambia yafuatayo kuhusu
“Talaka ni mara mbili. Kisha ni kumuweka kwa wema au kumwacha kwa ihsani...Na
Inafahamika kuwa kila Dini au ideolojia yoyote ina nidhamu yake ya kuendesha maisha kwa hali na njia iliyo nzuri. Bila ya nidhamu basi mahusiano hayatakuwa mema wala mazuri.
Kukiwa hakuna nidhamu na sheria madhubuti, mara nyingi itakuwa ni kuchezeana na katika kufanya hivyo mwanamke ndiye atakayeumia zaidi.
Mara nyingi mume huwa anamwambia mkewe kuwa yeye anampenda
1. Kuchunga nidhamu ya Dini na maadili yake.
2. Kuweka muruwa, heshima na mahusiano baina ya wanandoa.
3. Mume awe ni mwenye kujichunga asiwe ni mwenye kutoa talaka ovyo ovyo.
4. Kumchungia haki yule mwanamke aliye katika ndoa.
Na Allaah Anajua zaidi