Achari Ya Papai Bichi, Embe Mbichi Na Karoti
Achari Ya Papai Bichi, Embe Mbichi Na Karoti
Vipimo
Papai bichi - 1
Embe mbichi - 3
Karoti - 3
Pilipili mbichi - 7
Pilipili nyekundu ya masala/unga - 1 kijiko cha supu
Nyanya iliyosagwa (crushed) - 3 vijiko vya supu
Rai/chembe za hardali (mustard seeds) - ¼ kikombe
Majani ya mchuzi (curry leaves) - 2 miche
Methi (uwatu uliosagwa) - 2 vijiko vya cha chai
Haldi (bizari ya manjano) - 2 vijiko vya chai
Chumvi - kiasi
Ndimu - 3 (kamua maji)
Mafuta - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Menya papai, embe na karoti kisha katakata vipande virefu virefu kama vinavyoonekana katika picha.
- Katakata pilipili mbichi weka kando.
- Katika karai, weka mafuta yashike moto. Kisha tia rai zikaangike kidogo.
- Zinapoanza kurukaruka na kugeuka rangi, tia methi, majani ya mchuzi, pilipili mbichi, pilipili nyekundu ya masala ya unga na haldi na endelea kukaanga kidogo.
- Tia nyanya iliyosagwa endelea kukaanga kidogo.
- Tia papai, embe na karoti, endelea kukaanga, kisha punguza moto uwe mdogo mdogo.
- Mimina maji ya ndimu, ongeza kidogo maji yakihitajika yapate kuivisha papai, embe na karoti. Tia chumvi.
- Funika huku kila mara unafungua kugeuza geuza hadi iive. Onja, chumvi na viungo, ikiwa tayari.
- Kidokezo:
- Ukipenda ongezea achari ya embe ya mafuta ya tayari kijiko kimoja cha supuu izidi kutoa ladha ya achari.