Ikiwa Hana Ushahidi Kuwa Ni Bidhaa Za Mayahudi, Anaweza Kununua?
SWALI:
Assalaam Aleykum Warahmatullah Wabarakatu, kuna bidhaa
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kususa bidhaa za Mayahudi na wanaowasaidia.
Hakika ni kuwa suala hili halina utata kabisa, utata unakuja tu kwa kuwa sisi tumezoea bidhaa hizo kwa kiasi ambacho kuacha imekuwa ni mtihani kwetu. Kwa ajili hiyo tunajipatia udhuru mmoja na mwingine ili kuendelea kutumia bidhaa hizo.
Kanuni ya Uislamu iko wazi, kuwa tunatakiwa kushirikiana katika wema na ucha Mungu na kutoshirikiana katika uadui.
Allaah Aliyetukuka Anasema:
“Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu” (al-Maa’idah [5]: 2).
Na ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu) naye akasema: “Mwanaadamu ana maadui wa tatu: Adui yake, adui wa rafiki yake na rafiki wa adui yake”. Hawa ni maadui watatu ambao tunafaa tujihadhari nao
Kwa yaliyo juu ni dhahiri kuwa Waislamu wana wajibu mkubwa wa kuwasaidia ndugu zao Waislamu sehemu zote za ulimwenguni kwani wao kwa wao ni ndugu. Na kwa minajili hii, kushirikiana na kumfaidisha adui ili kumuua Muislamu ni jambo ambalo halifai kabisa. Ni madhambi makubwa zaidi kusaidia kumuua Muislamu kwa njia yoyote ile. Ndio Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
“Mnusuru nduguyo akiwa amedhulumu au amedhulumiwa”. Akaulizwa: “Yule aliyedhulumiwa tunafahamu lakini huyu aliyedhulumu tusamsaidiaje?” Akasema: “Muepusheni na dhuluma kwani kufanya hivyo ni kumnusuru” (al-Bukhaariy).
Kuwanusuru na kuwasaidia ndugu zetu ni kutumia njia nyingi
1. Kuwasaidia katika Jihaad yenyewe.
2. Kuwasidia kifedha ili waweze kujinasua na kujihifadhi kwa kuwa na silaha za kuweza kupambana na adui.
3. Kususia bidhaa za wenye kumsaidia adui na hii inakuwa ni wajibu wa kila Muislamu.
4. Kuwaombea du’aa kila wakati ili Allaah Aliyetukuka Awasaidie, kwani du’aa ni ‘Ibaadah.
Kwa kuwa kutumia vitu hivyo itakuwa ni kumsaidia adui ili kuwaua Waislamu, hivyo matumizi ya bidhaa hizo itakuwa haifai. Bidhaa za Israili huwa kawaida zinatengenezwa katika nchi na idhini
Yale yanayosemwa ni mambo ya hakika si mambo ya eti eti. Ushahidi ni ule unaotoka kwa mwenzio ambaye ni Muislamu na wala hana sababu ya kukudanganya. Na wao wenyewe lau ingekuwa si kweli wangejitetea kwa kuandika makala na kuyasambaza kama walivyoandika katika tovuti
Kisha Coca cola ina tatizo kuwa si kinywaji cha siha bali kina madhara makubwa katika mwili wa mwanaadamu jambo lililofanya bunge la
Kadhalika vinywaji vyote vinavyotengenezwa na kampuni hiyo
Pia Pepsi na wenzake kama Mirinda, Seven Up na zinginezo, zote hizo ni katika makampuni yanayohusiana na dola haramu la
Na pia kununua bidhaa katika maduka
Pia fatwa ya 1984 ya Majlis Ulamaa ya Afrika Kusini imeyakinisha kuwa vodka inatumika katika utengenezaji wa kinywaji hicho pamoja na dalili zao.
Tunakuwekea chini list ya bidhaa tulizojaaliwa kukusanya ambazo ima ni za Mayahudi moja kwa moja, au wana ushirikiano, hisa n.k.
MAKAMPUNI NA BIDHAA ZA MAYAHUDI ZA KUSUSIWA
AOL Time Warner |
|
Apax Partners & Co Ltd |
Coca-Cola |
|
Danone |
Delta Galil |
|
Disney |
Estée Lauder |
|
IBM |
Johnson & Johnson |
|
Kimberly-Clark |
Lewis Trust Group Ltd |
|
L'Oreal |
Marks & Spencer |
|
Nestle |
News Corporation |
|
Nokia |
Revlon |
|
Sara Lee |
Selfridges |
|
The Limited Inc |
Home Depot |
|
Intel |
Starbucks |
|
Timberland |
McDonald's |
|
Arsenal FC |
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atufanikishie mambo yetu ya kuweza kuwasaidia ndugu zetu kwa njia zote ikiwemo kususia bidhaa za Israili na washirika wake.
Na Allaah Anajua zaidi