Du'aa Katika Swalaah Za Sunnah Inafaa Kusomwa Kwa Lugha Nyengine Na Kimoyoni?

 

SWALI:

 

Assalaam alaykum Warahmatullah Wabarakatuh baada ya maamkizi hayo mema shukran zangu ziende kwa Mola wetu aliyetuumba Subhaana Wataala na pia alhidaaya. Sheikh nina maswali mengi kuhusu swala itakuwa vizuri kama utapata muda kunielimisha.

 

Dua ndani ya swala ya fardhi ni lazima kuisoma kwa lugha ya kiarabu je na weza kusoma dua kimoyomoyo ktk swala za suna kwa lugha ya kiswahili


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kusoma du’aa kimoyomoyo katika Swalah za Sunnah kwa lugha ya Kiswahili.

 

Hakika katika hilo inatakiwa mwanzo usome kwa kutamka du’aa kwa Kiarabu ambayo inajumlisha mambo mengi kamaRabbaana aatinaa fid Dun-ya Hasanatan wa fil Aakhirati Hasanatan wa Qina ‘adhaban Naar’, kisha utie Niyah moyoni kwa unachotaka. Huko kunaruhusiwa katika Swalah za Sunnah.

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi

 

Inajuzu Kuomba Du'aa Kwa Lugha Yoyote Katika Swalah?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share