Anataka Dalili Ya Kuwa Maimamu Wa Kishia Wanajipangia Wenyewe Kufa
Anataka Dalili Ya Kuwa Maimamu Wa Kishia Wanajipangia Wenyewe Kufa
SWALI:
Asalamun alaykum
Nashukuru kuhusu lile suali langu la kuhusu mashia kuwatukuza maimam lakini mm nimesomakam hivyo mlivyosoma nyinyi kuhusu hivyo vitabu vya kishia lakini hayo mmsijaoyaona sasa sijui nyinyi mmeyatoa wai na vile vile mnasema eti maimam hua wanajipangia wenyewe siku ya kufa mm hiyo sijaona naomba mnipatitie hicho kitabu kwani mm huwa nakwenda huko iran mara kwa mara lakini pia nimefuatilia saan mambo hayo lakini sijayaona na hata kua mnasema kua huyo Abdullah bin Sabaa ndie alienzisha huo ushia mm nimefanya tahkiki huku huku iran lakini sio kweli na nilisoma kitabu kilichoandikwa ujue ushie na nimesoma kwa vizuri tu lakini pia wao mwenyewe wanakanusha sasa wai niwakubali nyinyi au mashi naomba mkinijibu masuala yangubasi fanyeni tahkiki kwa uzuri zaidi kwani hatamnaweza pengine kuongeana shia mwenyewe sasa sijui mtafanya nini? Wa aleikum msalam salam kotoka znz.
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Hii hapa chini ni dalili na nyingine za ziada kwa faida:
1. Imam anajua wakati wa kifo chake na anachagua anavyotaka kufa (anakufa kwa kutaka kwake). [Usool-ul-Kaafi, Mjalada 2, Ukurasa 23, Iliyochapwa huko Iran]
Pia pokea na hizi nyongeza za kufru na upotofu uliomo kwenye hivyo vitabu vya Kishia.
2. Imamu wana elimu zaidi ya Rusuli (ina mapokezi zaidi ya 13) [rejea Bihaar al-Anwaar, mjalada wa 26, ukurasa wa 194 hadi 200]
3. Imamu ni wajuzi kuliko Rusuli, Manabii na vyote vilivyoumbwa. Rusuli wakubwa Nuwh, Ibraahiym, Muwsaa na ‘Iysaa wamepata daraja ya Uwlul-‘Azm kutokana na kuwapenda Maimamu [ina mapokezi 88]
4. Dua za Rusuli na Manabii zilijibiwa kwa sababu walizipitishia kwa Maimam [ina mapokezi 16]
5. Imam wana uwezo wa kufufua wafu. Wanaweza kutibu Upofu na Ukoma. Wana Elimu walizopewa Rusuli na Manabii [ina mapokezi 4]
6. Hakuna Elimu ya Mbinguni, Ardhini, Peponi na Motoni iliyofichwa kwao. Walioneshwa Ufalme wa Mbinguni na Ardhini. Wanajua yote yaliyotokea na yatakayotokea mpaka Siku ya Qiyaamah [ina mapokezi 22]
7. Imamu wanajua ukweli wa Imani ya Mtu au Unafiki wake. Wanacho kitabu cha Majina ya Watu wa Peponi, Majina ya Wafuasi wao na Maadui zao [ina mapokezi 40]
Kutokana na Sifa na uwezo wa Imamu wa Kishia inaonekana kwamba, wao sio Watawala au viongozi wa Kiroho tu bali wao pia ni wana uwezo na sifa kama za Rusuli na Manabii na licha ya yote dunia inawategemea kwa kila hali na kwa kuthibitisha haya Khomeini ameandika nadharia hii nzima kwa kuhalalisha mapinduzi katika kitabu chake Al-Hukumat al-Islamiyah.
8. “Ni nguzo ya Imani yetu isiyopingika kwamba Imamu wetu wana vyeo mbele ya Allaah ambavyo Malaika na Rusuli wanavitamani” (rejea kitabu hicho ukurasa wa 52)
Hayo kwa uchache ni upotofu na ukafiri uliojaa kwenye vitabu vya Kishia. Na unaweza kuvitafuta vitabu vyao hivyo kama:
Usuulul Kaafi
Man La Yahdhurul Faqiyh
Al-Istibsaar
Wasaail Ash-Shiy’ah
Bihaarul Anwaar
Kashful Asraar
Faslul Khitwaab Fiy Tahriyf Kitaabi Rabbil Arbaab
Haqqul Yaqiyn
Al-Hukuumat Al-Islaamiyah
Na vingi vinginevyo ambavyo utaona ndani ya vitabu hivyo.
Na Allaah Anajua zaidi