Makhalifa 12 Waliotajwa Kuwa Watakuja Ni Hao Maimaam 12 Wa Kishia Kama Wanavyodai Wao?
Makhalifa 12 Waliotajwa Kuwa Watakuja Ni Hao Imaam 12
Wa Kishia Kama Wanavyodai Wao?
SWALI:
Asalam Aleykum...Ningependa msaada wenu kuna rafiki yangu mshia alinipa kitabu kilichosema kwamba "kutakuwa na makhalifa kumi na mbili kutoka kwa Makuraysh/ Bani Hashim baada ya Nabiy (Swala Allaahu 'aleyhi wasalam)" pia hii hadiyth inapatikana katika kitabu cha hadiyth cha muslim. Sasa ao makhalifa ni wapi?? Na vipi kumuelewesha kwamba ao makhalifa kumi na mbili sio wao akina shia ithna ashariya...jazakallah.
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Hakika masimulizi hayo ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yako si katika Muslim tu, bali pia katika Swahiyh al-Bukhaariy na Sunan ya Abu Daawuud. Hata hivyo, katika Hadiyth zote hizo wametajwa Makhalifa wenyewe watatoka katika kabla la Quraysh na wala si ukoo wa Banu Haashim. Kumaanisha kuwa wanaweza kutoka katika ukoo wa Banu Haashim, Banu Makhzuum, Banu Mutwalib, Banu ‘Abd ad-Daar, Banu Umayyah, Banu ‘Adiy, Banu Taym, na kadhalika. Tufahamu kuwa koo za Quraysh zimegawanyika kuwa kumi na mbili.
Katika Hadiyth ya Muslim inasema:
"Dini ya Kiislamu itaendelea mpaka Saa (Qiyaamah) isimame au mmetawaliwa na Makhalifa kumi na mbili".
Ama Mashia, wao hawawaiti viongozi wao kwa jina la Khaliyfah bali Imaam ambao sifa zao ni za kiungu si za kibinaadamu. Kisha wao, hao Imamu wa kishia hawakuwahi kutawala na wala hawakufika 12 kama wanavyodai. Ila tu labda huyo wa 12 awe atazaliwa baadaye. Kwa nini tunasema hawakufika 12, ni kuwa Imaam wao wa 11, Hasan al-Askari hakuzaa kabisa. Kwa hiyo ni udanganyifu wao kusema kuwa Imaam wao wa 12 alizaliwa na yuko katika pango mpaka atakaporudi tena kueneza uadilifu kati ya wanaadamu duniani.
Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na manufaa zaidi:
Maimamu Wako Wangapi? Je Kuna Tofauti Baina Yao?
Anataka Dalili Ya Kuwa Maimamu Wa Kishia Wanajipangia Wenyewe Kufa
Na Allaah Anajua zaidi