Makundi Ya Twariyqah Ni Yepi Na Je Yanakubalika?

 

Makundi Ya Twariyqah Ni Yepi Na Je Yanakubalika?

 

Alhidaay.com

 

 

SWALI:

 

Asalaam Alaykum, Twalika Ni Nini Na Kina Nani Wanajinajibisha Na Kundi   Gani Na Je Matendo Yao Ni Ya Haki Au Bidaa

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Wa ‘Alaykumus Salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh

 

Tutakujibu kwa kifupi huku tukikuatia viungo hapo chini uvifungue na kusoma mada hizo zilizomo humo ndani zenye faida na maelezo kwa urefu.

 

Twariyqah ni njia ambazo makundi ya Kisufi yamejianzishia na hayana dalili yoyote kwenye Qur-aan wala Sunnah bali ni makundi ya kizushi yaliyoanzishwa kwa misingi ya kuzua na kutukuza watu.

 

Kuna makundi mengi ya hizo Twariyqah za Kisufi yenye majina mbalimbali, baadhi yake ni haya yafuatayo:

 

  • Qaadiriyyah
  • Shaadhiliyyah
  • Naqshabandiyyah
  • Dandarawiyyah
  • Suhrawardiyyah
  • Sanusiyyah
  • Mawlawiyyah
  • Tiyjaaniyyah
  • Badawiyyah
  • Burhaaniyyah
  • Chistiyyah
  • Darqawiyyah
  • Daasuqiyyah
  • Khalwatiyyah
  • Idrisiyyah
  • Isawiyyah

 

Yapo makundi mengi sana, na yote ni makundi ya uzushi yasiyo na asli katika Uislamu.

 

Na matendo yao mengi ni ya baatwil na uzushi na bid’ah; hayana asli wala dalili katika Qur-aan wala Sunnah.

 

Zaidi, tafadhali soma Makala zifuatazo hapa chini upate kufungukiwa zaidi:

 

1.    Usufi

 

2.    Kundi La Jama’at At-Tabliygh (Masufi)

 

3.    Jamaa'atu At-Tabliygh Na Muasisi Wake Aliyekuwa Mtu Wa Bid’ah

 

4.    Bid'ah - Uzushi Katika Dini

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

Share