Anampenda Mke Mdogo Zaidi, Anamsifia Sana Mbele Ya Mke Mkubwa, Je Ni Haki Hivi
SWALI:
Assalam aleykum warahma tullwahi wabarakat...
Suala langu ni kuhusu ndoa. Ikiwa mume kaowa mke mwengine japo atakua anampenda
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mume kumpenda mke mdogo zaidi kuliko yule mkubwa.
Uislamu umetoa ruhusa kwa mwanamme kuoa mke zaidi ya mmoja ikiwa ataweza kutekeleza uadilifu baina
Anafaa mume afanye juhudi kuwapenda wake zake wote sawa sawa wala hafai kuwatofautisha baina
Haifai Kiislamu kumtweza mwanaadamu yeyote awaye kwa mwenziwe. Kwa hivyo, hayo ni makosa na inafaa kwa mume aache hayo na badala yake ajenge mahusiano mema kwa wake zake wote wawili.
Pia haifai kuwafanyia mambo tofauti baina ya wakeze bali anatakiwa atekeleze uadilifu na usawa.
Bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi:
Mume Hatoi Haki Kwa Mke Wa Pili Kama Atoavyo Kwa Mke Wa Kwanza
Haki Za Mke Mkubwa Na Mke Mdogo
Na Allaah Anajua zaidi