Kuna Tofauti Ya Maana Katika Maneno Ya Ndoa?

SWALI:

 

Je kuna tofauti ya maana katika maneno haya Ndoa na Harusi

 

 

Natanguliza shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu Subhaana wa Taala na nyinyi pia ndugu zetu wa Alhidaaya. Wabillah Tawfiq

 

 


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Shukurani kwa swali lako kuhusu tofauti ya maneno katika Ndoa na Harusi. Ni kwamba  tofauti inaweza kuwepo baina ya maneno hayo mawili ya Ndoa na Harusi kutegemea mahali anapoishi mtu. Ndoa inatumika kwa maana kuoana kihalali kwa kufunga Nikaah ama harusi ina maana ya zile sherehe zinazofuatia. Ama katika sehemu nyingine hakuna tofauti baina ya ndoa na harusi.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share