Kuku Wa Kuchoma (Grilled) Wa Sosi Ya Haradali Na Slesi Za Viazi
Kuku Wa Kuchoma (Grilled) Wa Sosi Ya Haradali Na Slesi Za Viazi
Vipimo
Kuku - 5-6 Lb Mapaja na miguu
Kitunguu saumu/thomu iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Mtindi (Yoghurt) - 1 kijiko cha supu
Sosi ya haradali (mustard) - 2 vijiko vya supu
Sosi ya pilipili nyekundu - 2 vijiko vya supu
Ndimu - 2 vijiko vya supu
Chumvi - Kiasi
Jira (bizari ya pilau ya unga/cummin) - 1 kijiko cha chai
Gilgilani ya unga (coriander powder) - 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga - ½ kijiko cha chai
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Viazi - 4-5 vikubwa
Unga wa ngano - 2 vijiko vya supu
Mafuta ya kukaangia viazi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Safisha vipande vyako vya kuku kisha vichuje maji.
- Changaya viungo vyote kwenye bakuli
- Tia vipande vya kuku uchanganye na masala hayo kisha roweka kwa muda wa saa au zaidi. Kila akiroweka zaidi huzidi kukolea viungo.
- Menya viazi na vikate slesi za duara weka kando.
- Panga kuku katika treya na mchome katika oveni moto wa juu (grill) huku unageuza hadi kuku akaribie kuiva. Unaweza kumchoma kwenye jiko la mkaa vilevile. Akishaiva epua na panga kuku katika sahani.
- Tia viazi katika bakuli ulorowekea kuku litakuwa limebakisha sosi ya kuku uchanganye viaizi vizuri.
- Nyunyizia unga wa ngano katika bakuli la viazi, kisha vikaange kwenye mafuta mpaka viive, vitoe uchuje mafuta.
- Vipange katika sahani pamoja na kuku vikiwa tayari