Kamba Wa Kukaanga Kwa Toast
Kamba Wa Kukaanga Kwa Toast
Vipimo
Kamba wa maganda bila vichwa - 500 grams
Unga ngano - 1 kikombe cha chai
Yai - 1
Pilipili ya unga kijiko - ½ cha chai
Bizari ya manjano kijiko - ½ cha chai
Chumvi - kiasi
Mafuta Ya Kukaangia - kiasi
Namna ya Kutayarisha Na Kupika:
- Changanya yai, pilipili, bizari na chumvi kwenye bakuli.
- Osha kamba usiwatowe maganda, watoe vichwa.
- Ukishawaosha vizuri mimina kamba kwenye huo mchanganyiko, halafu mimina na unga.
- Bandika mafuta kwenye karai yakishakupata moto, kaanga kamba mpaka wawe rangi ya hudhurungi (golden brown). Moto uwe wa kiasi.
- Tayari kwa kuliwa na mkate au chips, au saladi.
