Kila Zikija Posa Baba Anazitia Ila Hata Haniulizi Mwenyewe Nami Nataka Kuolewa Nifanyeje?
SWALI:
A.a sheikhe nawapa shukran alihidaya kwa kuweza kuturekebisha na kutunfunza mambo yote yakidunia tulio na tashwishi nayo...jaza yenu iko kwa allah.me nimsichana 24, niko na shida moja kila nikija kuposwa haifiki mbali nitaona kimya hakuna tena lolote kuhusu ndowa.me natamani nianze maisha yangu ya ndowa lakini naona kheri zangu zina tashwishi. Babangu akija mtu kuniposa yeye lazima amtie mtu kasoro na ilaaa mpaka sasa
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu posa zinazo kuja na kukataliwa na babako kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe. Suala hili na shida uliyo nayo ni katika masuala nyeti
Inaonekana kuwa wazazi wameshindwa kuona tatizo
Mbali na ksuema hayo, mwanamke katika mas-ala ya ndoa ana haki ya kuulizwa na kukubali kuhusu mume atakaye kuwa wake wa mustakbali. Kwa hapa sisi tunaweza kukushauri yafuatayo:
1. Awali ya yote swali Swalah ya Istikhaarah, kumuomba Allaah Aliyetukuka Akubainishie kheri au shari ya huyu mume aliyekuja. Kisha naona umekosea
2. Ikiwa Istikhaarah imekuonyesha kheri ya huyo mume, jaribu kukaa na babako kwa njia muruwa ya heshima na uzungume naye kwa upole na hekima kuhusu suala la ndoa yako.
3. Ikiwa ni vigumu kwako kufanya hivyo zungumza na mamako ambaye atakuwakilisha kwa babako. Ikiwa si mamako mzazi basi watumie watu wengine ambao watazungumza na babako kama vile shangazi au ami au jamaa mwengine wa karibu ambaye anaweza kuzungumza na babako kuhusu suala
4. Waweza pia kumtumia Shaykh au mwalimu wa Madrasah amabaye anaaminiwa na babako ili kumzungumizia kuhusu
Hatuna shaka, ufumbuzi wa tatizo lako utapatikana kwa pia kuzidi kumuomba Allaah Aliyetukuka wakati unapofunga funga ya Sunnah, kuamka usiku na kuswali Tahajjud kisha kumuomba Yeye kwa unyekevu na wakati mwingine ambao du’aa zinakubaliwa kwa haraka.
Pia tungependa kukushauri utilie maanani
Na Allaah Anajua zaidi.