Vipi Wakimbizi Wajisafishe Na Uongo Wanaosema Serikalini?
SWALI:
ASALAMU ALYKUM
WENGI KATIKA SISI WAISLAMU TUMEHAMA MIJI NA NCHI ZETU NA KWENDA ULAYA, MAREKANI AU CANADA "KUTAFUTA MAISHA BORA"
HUKO ULAYA, MAREKANI AU
SWALI LANGU, JE, PESA HIZO NI HALALI? PILI URONGO HUO WATAFISIRIKA VIPI KIDINI? KAMA YOTE NI MAKOSA KIDINI YETU TUKUFU, JE NDUGU ZETU WATAJISAFISHA NA MAPESA HAYO YA HARAMU NA URONGO WA MIAKA MINGI?
WABILLAHI TOWFIQ
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu wakimbizi kujisafisha na uongo wanaosema serikalini.
Tufahamu kuwa mwanzo ukweli ni sifa muhimu
Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuarifu kuwa Muumini hawezi kuwa muongo kabisa.
Tufahamu kuwa pesa zinazopatikana kwa uongo si halali kwa mwenye kupatiwa kabisa. Wale waliopata pesa hizo inabidi wajisafishe na kwa hiyo waombe maghfira kutoka kwa Allaah Aliyetukuka. Katika kukubaliwa toba ni lazima mtu afanye yafuatayo:
1. Kujiondoa katika maasiya hayo. Kwa hiyo kuanzia sasa asiwe ni mwenye kuchukua tena pesa hizo.
2. Ajute
3. Aazimie kutolirudia tena kosa
4. Na kwa kuwa amechukua haki ya mwanaadamu ni lazima arudishe hicho alichochukua, katika swali hili ni pesa. Kwa kuwa huenda kuzirudisha moja kwa moja inaweza kumletea shida kutoka kwa serikali ni lazima atafute ya kuweza kuzirudisha kwa njia moja au nyingine.
Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:
Nasaha Kwa Wakimbizi Wanaoishi Kusema Hawajaoana Ili Wapate Ruzuku Ya Serikali
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atuepushe na uongo ili tusiingie katika matatizo hayo.
Na Allaah Anajua zaidi