Kisa Kwenye Barzanji Cha Kuzungumza Wanyama Wakati Alipozaliwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Sahihi?

SWALI:

 

Assalaam alaikum. ndugu wa alhidaaya kwanza shukrani sana kwa kupatikana website inao tupafaida mbali mbali. Na jaza yenu mungu atawalipa. Suali langu ni kuwa katika barzanji kwenye mlango "WALAMMA ARAADA LLAAHU TAALA".

 

Kuna ibara inasema kuwa wanyama wote wa maqureshi walisema kwa lugha ya kiarabu kuwa mimba ya mtume imebebwa. Na nimesikia shekhe moja akisema kuwa “imetoka kwa abuu nuaim kutoka kwa ibnu abaas radhi za mungu ziwafikie wote wawili wamesema moja katika dalili ya kubebwa mimba ya mtume wanyama wote wa bara la arabu walizungumza kuwa twaapa kwa mungu wa alkaaba, imebebwa mimba ya mtume nae ndie kiongozi wadunia na taa ya watu wake na vyeo vya wa falme wote vilianza kuyumba yumba kwa kuwa mtume anakuja. Wanyama wa mashariki wakakimbilia maghribi kutoa habari kuwa mimba ya mtume imebebwa. Kisa iki kimechajwa na alhaafidh al-askalani”. Suali langu nikuwa hiki kisa ni cha ukweli na wanyama ni kweli walizungumza? Shukran


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kuzungumza wanyama pindi mimba ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilipobebwa na mama yake.

Hakika hakuna ajabu kwa wanyama kuzungumza na katika uhai wake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alizungumza na wanyama na hata Nabii Sulaymaan (‘Alayhis salaam) alipatiwa miujiza hiyo ya kuzungumza na wanyama.

 

Hata hivyo, visa na miujiza mingi iliyotajwa kuwa ilitokea wakati wa kubebwa mimba na kuzaliwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hayana uthibitisho kabisa. Nyingi ni riwaya ima za kutungwa au dhaifu kama walivyosema wanachuoni wengi.

Na kuna vitabu vya Siyrah vizuri vya kusoma kuliko hiyo Barzanji, navyo ni kama ‘Ar-Rahiyqul Makhtuum’ cha Mubaarakpuri ambacho pia kiko kwa lugha ya Kiswahili, na pia kitabu kizuri cha mwenendo wa Mtume cha Imaam Ibnul Qayyim kiitwacho ‘Zaadul Ma’ad’ nacho kipo kwa Kiarabu na Kiingereza.

 

Na Allaah Aliyetukuka Anajua zaidi

 

Share