Yupi Bora Mbele Yake; Mama Au Mke?

 

Yupi Bora Mbele Yake; Mama Au Mke? 

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

A. Alaykum, 

 

Mimi suala langu ni hivi, tuchukulie km mimi ni mwanamme niliyeowa, na mke huyo ni mcha wa Allaah na mama yangu mzazi pia ni mcha wa Allaah, sasa kati ya hawa nani atakae kuwa bora?

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aaalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Hakika kama mume unatakiwa umpende kila mmoja katika hao wawili kwa mapenzi uliyoamuriwa na Shari’ah ya Kiislamu. Kila mmoja ana mapenzi yake haswa. Hata hivyo hufai kumpenda mke juu ya mama.  

 

 

Inatakiwa mkeo umpatie haki zake zote ambazo umelazimishwa na Shari’ah na vile vile mama lakini hufai kumtanguliza mke juu ya mama. Swahaba mmoja kwa jina ‘Alqamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alishindwa mwanzo kutamka shahada kwa sababu ya kumpenda mke zaidi ya mama. Aliweza kutamka tu shahada pale mama alipoamua kumridhia na kumsamehe yale yote aliyokosea (Ahmad).

 

 

Na hakuna badali ya mama lakini mke mnaweza kuachana na kila mmoja akapata wa pili wake mwengine. Hivyo, daraja ya mama iko juu ya mke na hata juu ya baba. Na Qur-aan pamoja na Hadiyth za Nabiy(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zimeelezea fadhila hizo nyingi.

 

  

Bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi: 

 

Mama…Kisha Mama…Kisha Mama

 

Haki Za Mume Na Mke

 

 

Na Allaah Anajua Zaidi

 

Share