Maana Ya Twahaarah
Maana ya Twaaharah
SWALI:
Twahara ni nini? Na inakuaje?
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Twahaarah kwa neno la usahali lenye kufahamika ina maana ya usafi. Hata hivyo, kishariy’ah ina maana zaidi ya usafi kwani katika Uislamu kitu au mtu anaweza kuwasafi lakini si twaaharah.
Kwa hiyo kishariy’ah kuwa na twahaarah ni ile hali ya kwamba mtu hana najisi na yuko safi kutekeleza ‘ibaadah kama ya Swalaah na nyinginezo zinazohitajia mtu kuwa twahaarah.
Kwa faidi ziyada bonyeza kiungo kifuatacho:
Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twaharaah
Na Allaah Anajua zaidi