Kuhusu Ndoto na Tafsiri Yake

SWALI:

 

Asala alaikum warahmatullah wabarakatu,

Swali langu ni hili: mimi nikiswali swala ya haja huwa mara nyingi naota kama nimefanikiwa kwenye mambo yangu lakini najikuta ni opposit, na sijuwi ni sababu gani.

 

Swala la pili napenda sana kuota ninasoma souratil fatha nawomba nipewe tafsiri ya ndoto hiyo pamoja na kuwota sana kama nawogota dhahabu.

 

Asalama alaikum warahmatullah wabarakatu


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuota ndoto na tafsiri yake.

Kabla hatujaingia katika lako tungependa kukufahamisha kuwa hakuna Swalah inayoitwa Swalaatul Haajah (au Swalaah ya Haja) kwani Maulamaa wamesema Hadiyth inayoeleza Swalah hiyo ni dhaifu na isiyokubalika, bali ile ambayo ipo ni Istikhaarah. Nayo inaswaliwa ikiwa Muislamu anataka kufanya jambo na hajui lipi ndilo la kheri.

Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

Je, Swalatul-Haajah Ni Sahiyh Na Ipi Duaa Yake?

 

Ama kuhusu maswali ya ndoto, hatuna elimu nayo, na hakuna wengi wanaoweza kutafsiri ndoto kwa wakati huu na wachache wanaojiingiza huko ni wale wasio wakweli. Hivyo tunakushauri usiwe unaendekeza sana ndoto na kuzifanyia kazi au kuzitafutia majibu yake, bali shughulika sana na mafundisho sahihi ya Diyn na yafanyie kazi yale uliyoamrishwa na Qur-aan an Sunnah na yaache yale uliyokatazwa nayo, utasalimika.

Hata hivyo, kuja kupata kitu kinyume na ulivyoota ni mtihani kutoka kwa Muumba wetu kukupima kama tutabaki katika Dini yake au utakwenda kinyume. Ikiwa utabaki na msimamo wako wa Diyn itakuwa kheri kwako hapa duniani na kesho Akhera. Ukienda kinyume na hivyo hasara itakuwa kwako.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share