Achari Tamu Na Kali Ya Karoti Na Nyanya/Tungule
Achari Tamu Na Kali Ya Karoti Na Nyanya/Tungule
Vipimo
Karoti - 5
Nyanya/tungule - 7
Kitunguu maji - 3
Pilipili mbichi - 3
Nyanya kopo (tomato paste) - 2 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7 chembe
Pilipili ya unga nyekundu - 2 vijiko vya supu
Mafuta - ¼ kikombe
Sukari - 2 vijiko vya supu
Ndimu - 3
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katakata vitunguu, nyanya, weka kando
- Kuna/puruza (grate) au katakata kitunguu thomu vidogodogo weka kando
- Katakata pilipili mbichi vipande virefu virefu weka kando
- Safisha karoti kisha katakata vipande virefuvirefu vya kiasi weka kando.
- Weka mafuta katika karai, kisha tia, kitunguu maji na cha thomu, nyanya, pilipili mbichi na ya unga, nyanya kopo (paste), chumvi. Vichanganye pamoja kabla ya kuweka katika moto.
- Weka katika moto mdogo, funika uive mchanganyiko. Usikoroge. Karibu na kukaanza kukauka tia karoti, sukari na ndimu, kisha ndio ukoroge kidogo kuchanganya.
- Acha katika moto kwa dakika moja tu ili karoti zisiive na kulainika, bali zibakie kuwa ngumu.
- Onja chumvi na ongeza pilipili na ndimu ukipenda iwe kali zaidi. Tayari kuliwa na chakula chochote upendacho.