Hind Mke Wa Abu Sufyaan Alisilimu Au Hakusilimu?
SWALI:
Asalam alekum mimileo nnasuala linanitatiza katika masomo yangu kuhusu huyu mke wa abusufiani yule alo utoa moyo wa khamza nakuula kwajina bibi hindu sualangu nihili yuyubibi alisilim au khakusilim naomba mnifahamishe nishauliza watu wengi wananambia kasili wengine wananambia khakusilim naomba mnifundishe
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran kwa swali lako kuhusu Bibi Hind bint Utbah (Radhiya Allaahu ‘anha).
Kwanza tunataka kukusahihisha kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa bibi huyu alikula ini (wewe umesema moyo) la Hamzah (Radhiya Allaahu ‘anhu). Hizo ni ngano za Kishia ambao wamechangia kuitengeneza ile sinema ya ‘The Message’ na kujaza uongo wao. Na yote ni kwa sababu ya chuki za Mashia kwa Abu Sufyaan na Hind (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwa sababu ni wazazi wa Mu’aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye hao Mashia na Makhawaarij wanamchukia na kumlaani Swahaba huyo mtukufu.
Mwanzoni bibi huyu alikuwa adui mkubwa wa Uislamu, lakini katika ule mwaka ambao Makkah ilifunguliwa yaani 8 Hijri/ 630 M alikuja mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasilimu kikweli kweli.
Na baada ya hapo alifanya mambo mengi mazuri ya Dini na kuutetea Uislamu na baadaye kufa akiwa Muislamu wa sawa sawa. Bibi Hind (Radhiya Allaahu ‘anha) ni miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Hivyo ndugu yetu kuwa makini katika kuisoma historia au wakati unaposimuliwa maana historia ya Uislamu imechafuliwa sana na maadui wa Uislamu wakiwemo Mashia na Makhawaarij.
Na Allaah Anajua zaidi