Baba Na Mama Waliotengana Anaweza Kumwandikia Mama Mali Kabla Ya Kufa Kama Zawadi?
SWALI:
Assalam aleykum,
Naomba kuuliza haki ya mirathi kwa Baba na Mama wazazi walikwisha tengana muda mrefu, Baba ana nyumba yake na ameshasema hata akifa Mama hana haki, mimi mtoto nikifa Baba na Mama kila mmoja ana haki kiasi gani kurithi vyangu iwapo mimi nitatangulia kabla yao.
Na Je kama sheria ya dini yeu inampa kipaumbele Baba hata
Najitahidi kutafuta kumsaidia Mama bila kuvunja sheria za dini yangu, Sheria ikimpa zaid Mama nikitangulia Mama atabakia anahangaika hana nyumba na ni yatima, na yeye hasa ndio aliyenijali kuliko Baba. Asanteni
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mirathi kwa wazazi.
Uislamu ambayo ni Dini ya kimaumbile inaweka shari'ah ya kila mtu na kila mtu anapewa haki yake. Kuhusiana na mirathi ni kuwa pindi wazazi (mume na mke) wanapoachana na eda ikamalizika ya mama yako hawatoweza kurithiana kishari'ah kwa sababu mafungamano
Ama kuhusu
Allaah Aliyetukuka Anasema:
“Na wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi ya alichokiacha, ikiwa anaye mtoto. Akiwa hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja. Na akiwa anao ndugu, basi mama yake atapata sudusi” (an-Nisaa’ [4]: 11).
Kwa hiyo, kulingana na Aayah ya hapo juu ni kuwa:
1. Ukiwa na watoto, kila mzazi wako (baba na mama) atapata sudusi (1/6).
2. Ikiwa wazazi ni warithi peke yake, baba atapata thuluthi mbili na mama thuluthi.
3. Ikiwa una ndugu waliobakia nawe basi mama atapata sudusi.
Ama kumsaidia mama yako ni jambo zuri na la thawabu kubwa
Na Allaah Anajua zaidi