Saladi Ya Matango, Capsicum, Nyanya Dressing Ya Parsley
Saladi Ya Matango, Capsicum, Nyanya Dressing Ya Parsley
Vipimo
Saladi ya uwa (lettuce wrap/iceberg) - 1
Matango - 3
Pilipili boga (capsicum) - 2
Nyanya/tungule - 4
Namna Ya Kutayarisha
- Chambua saladi, osha kisha chuja maji, kisha katakata na weka katikati ya sahani ya saladi.
- Katakata nyanya/tungule zungushia pembeni yake.
- Katakata tango zungushi pembeni ya nyanya/tungule.
- Katakata pilipili boga (capsicum) weka katikati ya saladi.
Vipimo vya Sosi Ya Saladi ya Parsely (Parsely salad dressing)
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 chembe
Parsley (aina ya kotmiri) kavu - ¼ kikombe
Pilipili manga au nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai
Mafuta ya zaytuni (olive oil) - ¼ kikombe
Siki au ndimu - 3 vijiko vya supu
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha
- Chuna (grate) au saga kitunguu thomu, kisha weka katika kibakuli.
- Changanya na viungo vilobakia.
- Wakati wa kula, mwagia juu ya saladi.
- Kidokezo:
- Ukikosa parsley kavu, tumia freshi.