Saladi Ya Tabbulah 1 - Lebanon
Saladi Ya Tabbulah 1 - Lebanon
Vipimo na Namna ya Kutayarisha
Parsley (aina ya kotmiri) osha, chuja maji katakata (chop) - 4 misongo (bunches)
Nanaa (mint leaves) - 1 msongo
Vitungu majani (spring onions) katakata vidogodogo - 7
Kitunguu maji - 2
Tungule nyanya ya kawaida - 3 kubwa
Matango – 3
Burghur (ngano ilokobolewa) Tazama picha - ¼ kikombe
Limau kamua - 2
Chumvi – kiasi
Mafuta ya zaytuni - 1/3 kikombe
Namna Ya Kutayarisha
1. Osha bulgur tia maji roweka muda robo saa, kisha ichuje maji na ukamue itoke maji yote.
2. Katika bakuli weka vitu vyote isipokuwa limau, chumvi na mafuta ya zaytuni.
3. Karibu na kupakua changanya bulgur, limau na mafuta ya zaytuni katika kibakuli kidogo kisha mwagia na changanya pamoja na vitu katika bakuli.
Kidokezo:
Hakikisha umechuja maji majani na vitu vyote kwani Tabbulah hulegea mara moja. Na pia ni vyema kuchanganya vitu karibu na wakati wa kupakua