Wudhuu Unatenguka Akipeana Mkono Au Kugusana Na Asiye Muislamu?
Wudhuu Unatenguka Akipeana Mkono Au kugusana Na Asiye Muislamu?
SWALI:
Kupeana mikono kwa kusalimiana na mtu mwanaume mwenzangu lakini si muislamu (mkristo) inatengua udhu?
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kupeana mkono na asiyekuwa Muislamu hakutengui wudhuu kabisa kwa si miongoni mwa mambo yenye kutengua wudhuu.
Huenda watu wengine wakafikiria hilo kwa kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameiwaita ni najisi katika Suwrah At-Tawbah lakini najisi walio nayo ni ule ushirikina wao wala sio unajisi kama ule unaojulikana kama wa mkojo, kinyesi na vitu vinginevyo.
Bonyeza viungo vifuatavyo upate faida zaidi kuhusu Twahara kwa ujumla na yanayotengua na yasiyotengua wudhuu:
Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twaharaah
031-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Yanayotengua Wudhuu
032-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Mambo Yasiyotengua Wudhuu
Na Allaah Anajua zaidi