Mke Na Mume Wameachana Kisha Wakaingiliana Wakati Wa Eda Je, Watakuwa Wamerudiana?
SWALI:
A/Aleykum, naomba kuuliza swali, mke na mume wakiachana wakiwa kwenye kipindi cha eda wakiingiliana kwa hiyari yao wala hawakulazimishwa jee wanakua wamerudiana? nitashukuru sana mkinifumbulia hili swali
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu wanandoa kujamiiana wakati wa eda.
Hakika ni kuwa lengo la eda katika shari’ah ni kuwapatia fursa wanandoa kuweza kuzingatia waliyoyafanya na kurudiana ili wawe katika ndoa.
Na kufanya sahali huko kwa shari’ah kuweza kurudiana ndio kukapatikana kuwa mwanamke hafai kuhama katika nyumba aliyokuwa akiishi ili mume awe anamuona kila wakati. Na mke anafaa ajipambe ajipambe ili kumvutia mume wake
Mume akishamuingilia tu basi huko kutakuwa ni kumrudia. Kurudiwa huko kutakuwa hakuna mahari mpya wala nikaah japokuwa talaka moja itakuwa imeshapita.
Kwa maelezo na manufaa zaidi, tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo:
Niko Kwenye Eda Ya Talaka Naweza kurudiana Na Mume Wangu?
Mume Kaniingilia Wakati wa Eda – Hatimizi Sheria Za Kunihudumia??
Mke Kukutana Na Mume Baada Ya Eda
Na Allaah Anajua zaidi