Wapi Kuelekea Qibla Katika Nchi Ya Holland?

SWALI:

 

 

suali langu ni kuwa mimi naishi Holland na takriban watu wengi

wanaelekea qibla upande wa mashariki linapotoka juwa je ni sahihi kama si

 

sahihi naomba unijulishe qibla ni upande gani?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 Shukurani kwa swali lako kuhusu Qibla nchi ya Holland.

 

 

Ni kweli ya kwamba watu wanao swali kwenye msikiti wanaelekea Mashariki na ndiko jua linapotoka.

 

Lakini qiblah haswa ni huko Mashariki uongeze kidogo kulia kwako kwenye kuelekea.

 

Kwanini watu wamelekea Mashariki moja kwa moja?

 

Hili linatokana na plan za miji.  Ujenzi wa misikiti yenyewe imejengwa kwani takribani misikiti yote [isipokuwa michache tu] ni majumba ambayo yamejengwa kwa ajili ya makazi na baadaye yakageuzwa kuwa misikiti , hivyo maamuma wanapanga swafu zao kutokana na jengo lilivyo yaani kuelekea Mashariki lakini imaam huwa anapinda kidogo yaani upande wa kulia kwa Mashariki ambapo ndio kuna qiblah haswa.

 

Na kwa usalama zaidi ni vyema ununue ‘dira’ kwenye maduka ya Kiislamu itakusaidie kukujulisha Qibla kilipo hasa.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share