Makumi Matatu Ya Ramadhwaan Na Yepi Kufanya
Makumi Matatu Ya Ramadhwaan Na Yepi Kufanya
SWALI:
Aslaam alayku!
Naomba kupata ufafanuzi wa makumi yoote matatu na taratibu nzuri za kuyataekeleza nayanayotakiwa katika makumi haya matatu ya mwezi wa Ramadhan.
Ishaalah
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ramadhwaan ni mwezi mtukufu wenye fadhila nyingi, na siku zake zote ni sawa na nyingine, isipokuwa kumi la mwisho ambalo ndani yake kuna siku ya Laylatul-Qadr, siku ambayo ibada yake ni bora kuliko miezi elfu.
Hakuna dalili iliyothibitika kuwa kuna ibada khaswa ya kutekeleza katika makumi matatu ya mwanzo.
Hivyo siku nyingine zote au makumi mengine yote hayana tofauti katika fadhila za mwezi huu, bali ni kutekeleza Swawm ipasavyo, kuswali Qiyaamul-Layl (kusimama kisimamo cha usiku kuswali) na kufanya mengi ya kheri na kuzidishi Taqwa (Uchaji Allaah) n.k.
Tafadhali ingia katika kiungo kifuatacho kusoma yanayopasa kufanya katika kumi la mwisho:
Siku Kumi Za Mwisho Za Ramadhwaan
Laylatul-Qadr- Vipi Tunaweza Kuupata Usiku Huu?
Na Allaah Anajua zaidi