Pilau Ya Mpunga Kwa Nyama Ya Ng’ombe
Pilau Ya Mpunga Kwa Nyama Ya Ng’ombe
Vipimo
Mchele (mpunga unaonukia) - 4 vikombe
Nyama - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 3
Mbatata/viazi - 7 vidogodogo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa 3 vijiko cha supu
Bizari nzima/ya pilau/uzile/cumin - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 3 vipande
Hiliki - 7 punje
Pilipili manga nzima - 1 kijiko cha supu
Chumvi kiasi
Mafuta - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha mchele weka kando
- Katakataka vitunguu slice ndogo ndogo.
- Weka mafuta katika sufuria kisha ukaange vitunguu pamoja na mdalasini, hiliki pilipilimanga.
- Vitunguu vikigeuka rangi unatia kitunguu thomu na tangawizi.
- Tia supu kidogo na nyama, kisha tia bizari ya pilau/uzile, na viazi/mbatata.
- Maliza kutia supu yote, na ikiwa ni kidogo ongeze maji kiasi cha kuivisha mchele. kisha tia mchele ufunike hadi wali uwe tayari.
- Ikiwa unatumia mkaa palia juu yake, ikiwa hutumii uache uive kwa moto mdogo mdogo.