Wali Wa Mboga Mchanganyiko Kwa Mayai Ya Kuchemsha
Wali Wa Mboga Mchanganyiko Kwa Mayai Ya Kuchemsha
Vipimo
Mchele (Basmati) - 3 vikombe
Mbogamboga za barafu
(karot, njegere, spring beans na mahindi) - 1 kikombe
Kuku Kidari - 1 LB (ratili)
Mayai - 2 mayai
Vitunguu (vikubwa) - 2 au 3 vidogo
Pili pili manga - 1 kijiko cha chai
Paprika - 1 kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Mafuta - 1/3 kikombe cha chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu
Tangawizi - 1 kijiko cha chai
Kidonge cha supu - 1
Soy sauce - 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku
- Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.
- Tia mafuta kidogo katika wok (aina ya karai)
- Kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.
- Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.
Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali
- Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.
- Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi
- Wacha uchemke asilimia 70%
- Chuja maji na weka kando
- Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu
- Kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka (crumbled egg)
- Changanya mchanganyiko wa kuku na mboga
- Kisha tia wali changanye vizuri
- Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive
- Kisha pakua katika sahani na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.