Ndoa Inafaa Baada Ya Kumchezea Mwanamke?


 

  

SWALI:

assalam alaikum nashkuru sanaa kwa kunijibu maswali yangu lakini nna mushkeli mwen gine mimi nna mchumba wangu nna nia yakumuoa laikini huwa ananilazimisha tufanye machafu sasamimi huwa nnakataa lakini siku moja alinihadaa akaniambia twende beach  samahani shekh nakueleza ukweli nilipofika nikapata bilis nilimchezea kila sehem  akavua nguo zake karibu zote lakini sikumuingilia jee itafaa kumuoa kwani nnampenda sanaa na sitaki kufanya halamallam alla akulipeni kwa kutusaidia duniani na kesho akhera

 


 

JIBU

  بسم الله الرحمن الرحيم الحمد لله والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وعلى آله وصحبه أجمعين و بعد

Kwanza tunapenda na sisi kutoa shukurani kwa Du'aa zenu nzuri mnazotuombea nyote mnaotuma maswali yenu pamoja na wengineo wanaoingia ALHIDAAYA kutafuta faida mbali mbali. Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atutakabalie hizo Du'aa na Atuzidishie uwezo wa kuelemishana kwa kadiri Anavyotujaalia. Aamiyn.

Hakika tunasikitika kuona kwamba dada zetu wengine wako tayari kujiharibia maisha yao kwa kutaka kufanya vitendo vya maasi kama huyo dada aliyekulazimisha ufanye naye mambo machafu.

Tutambue kwanza kwamba Uislamu umekataza kuwa na mchumba (boyfriend/girlfriend) jambo ambalo ni katika mila za makafiri na sio katika mafundisho ya dini yetu. Allaah سبحانه وتعالى Ametuonya kufanya hivyo:

((وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلاَ مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ وَمَن يَكْفُرْ بِالإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِين))

((Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapowapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anayekataa kuamini bila shaka a'mali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara)) [Al-Maaidah: 5]

Na kufanya hivyo yaani kuwa na mchumba na kukutana naye huenda mtu akatawaliwa na ibilisi kama ilivyokuwa katika hali yako na kuingia katika maasi ya zinaa.

Unapasa kumshukuru Allaah سبحانه وتعالى kuwa Amekuzindua kupukana na iblisi kabla ya kumuingilia kabisa pengine ingeishia kubeba huyo mwanamke mimba ya haraamu.

Madamu unanampenda kama unavyosema, basi ni bora kwako kukimbilia kumuoa haraka iwezekanavyo ili uwe naye kihalali na yeye pia atulize matamanio yake kabla ya ibilisi kukuvaeni  na kukuingizeni katika maasi tena.

Inafaa kabisa kumuoa bila shaka yoyote ila tu mnatakiwa nyote muombe Tawbah kwa Mola wenu kwani Allaah سبحانه وتعالى Hupokea Tawbah ya aina yoyote kutoka kwa mja Wake kama Anavyosema:

 ((إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللّهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوَءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُوْلَـئِكَ يَتُوبُ اللّهُ عَلَيْهِمْ وَكَانَ اللّهُ عَلِيماً حَكِيماً))

((Hakika toba inayokubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu Huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na ni Mwenye hikima)) [An-Nisaa 17]

Vile vile Mtume صلى الله عليه وآله وسلم anasema kuwa tawbah inakubaliwa madamu mambo mawili yaliyotajwa katika Hadiyth hizi mbili hayakumfikia bado mja,

Jambo la kwanza:

  ((إن الله يقبل توبة العبد ما لم يغرغر)) رواه أحمد والترمذي وصححه النووي

((Hakika Allaah سبحانه وتعالى Huikubali tawbah ya mja Wake kabla ya roho kufika kwenye mkoromo wa mauti))  Imesimuliwa na Ahmad na Kusahishwa na An-Nawawy

Jambo la pili:

 عن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صل قال: ((من تاب قبل أن تطلع الشمس من مغربها تاب الله عليه))  رواه مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema,  ((Atakayetubu kabla ya kuchomoza jua upande wa Magharibi, Allaah سبحانه وتعالى Atamkubalia tawbah yake)) [Muslim] 

Tunarudia nasaha yetu muhimu ya kukuomba ufanya haraka kufunga ndoa na huyo msichana ili nyote muweze kutimiziana matamanio yenu kwa njia ya halaali na pia mumridhishe Allaah سبحانه وتعالى   

Wa Allaahu A'alam

 

 

 

 

 

Share